Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Reuben Shigela alipotembelea Kampuni inayotarajiwa kujenga mradi mkubwa wa kiwanda cha Saruji Jijini Tanga. Kiwanda hicho muhimu kwa uchumi wa Tanzania kitazalisha zaidi ya tani milioni 7 za Saruji kwa mwaka.
Mhe. Martin R Shigela Mkuu wa Mkoa wa Tanga alienda Nchini China kwa mwaliko wa Serikali ya China kuhudhuria Mkutano wa One Belt One Road uliofunguliwa na Rais wa China Mhe. Xi Jinping.
Katika Mkutano huo Mkoa wa Tanga ulitarajia kupata faida kubwa kwani mkataba wa kujenga kiwanda kikubwa cha Saruji Mkoani Tanga chenye uwezo wa kuzalisha tani milioni 7 za Saruji kwa mwaka na kuzalisha ajira 4,000 ulitarajiwa kusainiwa na pande mbili za China na Tanzania.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.