Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Reuben Shigela katika muendelezo wa ziara za kutembelea Wilaya zote Mkoani Tanga, alitembelea Wilaya ya Lushoto tarehe 06/07/2017 kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi. Katika ziara hiyo Mhe. Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa Eng. Zena A. Said pamoja na viongozi wengine kutoka Sekretarieti ya Mkoa. Mhe.Mkuu wa Mkoa aliweza kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia majibu akishirikiana na timu aliyoambatana nayo kutoka Mkoani pamoja na wenyeji wake ambao ni Mkuu wa Wilaya ya Lushoto na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya za Lushoto na Bumbuli. Pia Mkuu wa Mkoa alitoa mikopo kwa Vikundi mbalimbali vya akina mama, (fedha hizo za mikopo zinatokana na mapato ya ndani kutoka kwenye Halmashauri husika). Pia katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alikutana na mabaraza ya Madiwani kwa ajili ya kujadili hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali ikiwa ni pamoja na kukutana na Wananchi na kusikiliza kero zao. Mhe. Mkuu wa Mkoa Pia alipatana nafasi ya kuwapongeza Wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano ya kitaifa yaliyofanyika Jijini Mwanza mwaka huu.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.