BODI ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imewasili mjini hapa kutembelea Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), pamoja na mambo mengine, kukagua, kubaini na kuzipatia shuluhisho changamoto zilizopo kwenye mradi huo.
Ujumbe wa Bodi hiyo ulioongozwa na Mwenyekiti wake, Profesa Mark Mwandosya, kabla ya kwenda kwenye eneo la mradi, umekutana na kuzungumza na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian ofisini kwake leo Juni 2, 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt James Andilile, amesema lengo la ziara hiyo, ni kutembelea EACOP na kujionea hatua za utekelezaji wa mradi huo, pamoja na changamoto zilizopo ili ziweze kushughulikiwa kwa wakati.
“Tumeamua kutembelea mradi huu muhimu kwa ajili ya ufuatiliaji wa karibu, kuhakikisha changamoto zinatatuliwa mapema na mradi unakamilika kama ilivyopangwa,” amesema Dkt. Andilile.
Aidha, ujumbe huo wa EWURA umepanga kukutana na wadau mbalimbali wa sekta ya nishati mkoani humo, ili kusikiliza maoni yao kuhusu namna bora ya kuboresha utekelezaji wa miradi ya kimkakati kama EACOP.
Bodi hiyo pia imepongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika kuhamasisha maendeleo na uwekezaji mkoani humo, ikitolea mfano wa Hati Fungani ya Kijani ya Tanga Uwasa, ambayo imekuwa mfano bora wa mafanikio katika soko la fedha nchini.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.