• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

RAS MCHATTA 'AWAFUNDA' WATUMISHI TANGA AKIHIMIZA UFANISI, TIJA

Imewekwa tarehe: January 29th, 2026

Na Mashaka Mgeta, SAADANI


UMBALI wa takribani kilomita 131 kutoka jijini Tanga, inapatikana Hifadhi ya Taifa ya Saadani, mahali palipofanyika kikao cha Baraza la Wafanyakazi mkoani Tanga Januari 27 na 28, 2026.

Wajumbe wa kikao hicho kutoka wilaya nane za Mkoa wa Tanga, wamekutana kwenye hifadhi hiyo yenye upekee wa kuwa ufukweni wa Bahari ya Hindi.

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Rashid Mchatta, anafungua kikao hicho kwa kuwahimiza watumishi wa umma kuwekeza zaidi kwenye utendaji kazi wenye tija na ufanisi kupitia utoaji huduma kwa jamii.

Mchatta anasema Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, inatimiza wajibu msingi wa kuwalipa watumishi stahiki zao inavyostahili na kwa wakati, hivyo ni jukumu lao (watumishi) kuitafsiri hali hiyo kama deni linalopaswa kulipwa kupitia utendaji kazi wao.

“Mazingira yaliyopo kwa watumishi wa umma ni wezeshi, yanayotoa hakika ya kufanya kazi ili kufikia malengo ya kuwatumikia wananchi…hili deni tunalipaswa kulilipa kwa kufanya kazi kwa ufanisi ili tija ipatikane,” akasema.

Pia, Mchatta amewaasa watumishi katika Sekretarieti ya Mkoa huo, kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kubuni fursa mpya za uwekezaji na miradi itakayochangia kuinua pato la taifa, kuboresha na kustawisha maisha ya watu.

Naye Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE) wa Mkoa wa Tanga, Straton Lufyagila, ameiongoza Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga kwa kufanikisha kikao hicho, na kufanikisha kuwa cha wazi, haki na usawa katika kujadili masuala yanayowahusu watumishi.


Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • JAJI MFAWIDHI TANGA ANENA: MIFUMO IMEDHIBITI RUSHWA, UKIRITIMBA MAHAKAMANI

    February 02, 2026
  • RC TANGA ATAJA MAENEO YA USHIRIKIANO NA MAHAKAMA

    February 02, 2026
  • COPRA YAGAWA TANI 1.35 YA MBEGU ZA UFUTA TANGA

    January 30, 2026
  • BAADA YA RS TANGA: SAADANI YAZIITA TAASISI KUFANYA VIKAO KWENYE HIFADHI

    January 30, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.