Na Mwandishi Wetu, OMM TANGA
KATIBU Tawala Mkoa (RAS) wa Tanga, Pili Mnyema amewataka watendaji wa halmashauri za mkoa huo kukaa ndani ya maeneo na vituo vyao vya kazi, ili kurahisisha utendaji kazi na kuwahudumia wananchi kwa karibu na ufanisi zaidi.
Mnyema, amesema hayo wakati akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza Maalumu la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga wa kupitia hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
'Unapovutiwa kwenda kukaa eneo tofauti na unapofanyakazi, akili yako hautaielekeza kwenye eneo unalofanyia kazi, muda mwingi utakuwa unawaza niwahi kutoka, niwahi kurudi nyumbani, lakini pia utachelewa kuingia ofisini na muda wa kufikiri mipango mizuri ya kuimarisha halmashauri utapungua," amesema
Akiwa kwenye baraza la Halmashauri ya Jiji la Tanga, Mnyema amewataka watendaji kufanya kazi kwa uaminifu, uadilifu na kujituma katika kipindi ambacho mabaraza ya madiwani yatavunjwa ili kupisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu wa 2025.
"Niwaagiza watumishi, katika kipindi ambacho mabaraza ya madiwani yatavunjwa, mfanyekazi kwa uaminifu, uadilifu, kujitoa kwa nguvu na akili zaidi ili kuhakikisha mipango mliyoiweka wakati madiwani wapo inakwenda kwa kasi kubwa, ili wakirudi wasikute jambo lolote limekwama,”amesema.
Pia, Mnyema ameonya kuwa watumishi hao wasitumie hali ya kutokuwepo kwa madiwani kama fursa hii kufanya mambo yasiyofaa kwa sababu madiwani ambao ni mfano wa jicho linalowaangalia wameondoka.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.