KATIBU Tawala Msaidizi (Utawala na Rasilimali Watu) wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga, Sebastian Masanja, amewashauri waajiri kujenga utamaduni wa kuzungumza na watumishi wao ili kubaini changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Masanja ametoa wito huo wakati akihitimisha Mkutano Mkuu wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania, ambapo amesisitiza kuwa waajiri wanapaswa kuwatunza na kuwalea watumishi wao, sambamba na kuzitambua changamoto kabla ya kuchukua hatua za kinidhamu kama kufukuzwa kazi.
“Ni muhimu kwa waajiri kuwa karibu na watumishi wao, kusikiliza matatizo yao na kushirikiana kutafuta suluhisho. Hii itapunguza migogoro ya kikazi na kuongeza ufanisi,” alisema Masanja.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu wa Afya Tanzania, Juliana Mawalla, alieleza kuwa makatibu hao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, kubwa ikiwa ni uhaba wa watumishi katika nafasi hiyo, hali inayosababisha mzigo mkubwa wa kazi.
Mkutano huo uliwakutanisha makatibu wa afya kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujadili mikakati ya kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi katika sekta ya afya.
10:40 AM
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.