Mkuu wa mkoa wa Tanga Omary Mgumba amekabidhiwa Shule ya Msingi ya Mahitaji Maalum ya Pongwe Jijini Tanga, iliyofanywa ukarabati mkubwa wa miundombinu yenye thamani ya Tshs.Milioni 220 kwa msaada wa Taasisi ya Lady Feteemah Trust kutoka nchini Uingereza.
Akiishukuru Taasisi hiyo katika sherehe fupi ya kukabidhiwa (Jana jumapili Oktoba 9, 2022) Mkuu huyo alisema kuwa hakika ukarabati huo utaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum pamoja na walimu hapa shuleni.
Serikali inayoongozwa na Rais Samia Hassan inawashukuru kwa ukarabati mkubwa wa madarasa 16, kiwanja cha Goal Ball, Bwalo la chakula na jiko, chumba cha huduma ya kwanza, ujenzi wa madarasa 2 mapya, kisima kirefu cha maji, sehemu ya kuchezea watoto walemavu na matundu 5ya vyoo vya walimu" ameshukuru Mgumba.
Amesema kwa hilo Serikali inatambua msaada huo na kwamba miundombinu hii itatunzwa ili iweze kudumu kwa kipindi kirefu.
"Natoa wito kwa viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Jiji la Tanga pamoja na jamii yote ya shule ya msingi kuhakikisha tunaitunza vyema miundimbinu hii iweze kudumu, watoto wetu wa some katika mazingira mazuri" alisisitiza zaidi.
Shule ya msingi Pongwe ambayo kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 1212, ni miongoni mwa shule kongwe nchini ikiwa imeanzishwa mwaka 1946.
Mwisho
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.