Serikali mkoani Tanga imesema kuwa imejidhatiti kukabiliana na ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka katika nchi ya jirani ya Uganda hivi karibuni.
Akizungumza katika Kikao Kazi cha Wakuu wa Wilaya na Mkoa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tanga Dkt. Jonathan Budemu amesema tayari Timu ya Wataalam ìshaandaliwa kuwafanyia uchunguzi watu wanaoingia, vifaa maalum na kutenga eneo la kuwatibu wagonjwa hao.
"Kwa sasa Halmashauri zote 11 hapa Tanga zimeandaa timu ya Dharura (Rapid Respond Team) iķiwa na wataalam watatu kwa kila kitengo na kuainisha maeneo ya kuwaweka na kuwatibu wagonjwa hao, Mpakani Horohoro kuna mabanda mawili ya wanaume na wanawake kwa ajili ya uchunguzi kwa wageni wanaoingia" alifafanua zaidi.
Aidha Dkt Jonathan amewataka wananchi kutoa taarifa katika vituo vya afya au watendaji wa vijiji endapo kuna mtu mwenye dalili za ugonjwa huo ambayo ni homa kali kwa ghafula, kutapika, kuharisha na kutokwa kwa damu sehemu za wazi.
Amesema chanzo cha ugonjwa huo hatari ni kula nyama za nyani, swala na mizoga ya wanyama, hivyo ni vema kutopeana mikono na kunawa mikono mara kwa mara na sabuni.
Mwisho
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.