MWENGE WASHAURI ELIMU YA RUSHWA IJIKITE KATIKA KUZUIA
Na Mashaka Mgeta, KILINDI
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, amehimiza elimu ya rushwa kwa jamii, hususani watoto na vijana, ijikite katika stadi za kuzuia zaidi ya kupambana na vitendo hivyo vinavyoathiri ufanisi katika utumishi wa umma na sekta binafsi.
Mnzava ameyasema hayo leo, baada ya Mwenge wa Uhuru 2024 kukagua na kuzungumza na wanachama zaidi ya 100 wa klabu ya wapinga rushwa na dawa za kulevya katika Shule ya Sekondari Mbwego iliyopo wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, kisha kuzindua klabu hiyo.
Kwa mujibu wa Mnzava, hatua hiyo itachangia kuwa na kizazi kinachopinga rushwa kwa dhamira ya dhati na mioyo iliyo wazi kuichukia, kuikataa na kuifichua (rushwa) mahali popote.
Naye Mwenyekiti wa klabu ya wapinga rushwa na dawa za kulevya katika Shule ya Sekondari Mbwego, Solomoni Isaya, amesema klabu hiyo imeanza kutumia jina hilo Machi 2024, ikitokana na klabu ya awali ya wapinga rushwa iliyoanzishwa shuleni hapo mwaka 2012 ikiwa na wanachama 42.
Solomoni ameuambia Mwenge wa Uhuru 2024 wenye ujumbe unaosema ‘’Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Ujenzi wa Taifa Endelevu’’ kuwa hivi sasa, klabu hiyo ina wanachama 162, wavulana wakiwa ni 70 na wasichana 92.
Kwa mujibu wa Solomoni, wanachama wa klabu hiyo wanapata elimu kuhusu mapambano dhidi ya rushwa na dawa za kulevya kupitia vipeperushi, majarida na masomo mbalimbali yanayotolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Solomoni amesema, klabu hiyo inashiriki shughuli mbalimbali za uelimishaji umma kuhusu athari za rushwa na dawa za kulevya kwa nyimbo, mashairi, ngojera, uandishi wa insha, kufanya maonyesho na kuwashirikisha wazazi, walezi na wanafunzi wenzao kuhusu madhara ya rushwa.
Kwa upande mwingine, Mwenge wa Uhuru 2024 ulikagua na kuridhishwa na uendelevu wa miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2023, kuzindua darasa moja lililopo katika Shule ya Sekondari Mbwego lililogharimu Shilingi milioni 20 zilizotolewa na Serikali Kuu huku nguvu za wananchi zikiwa ni Shilingi 700,000.
Ukiwa katika wilaya ya Kilindi, Mwenge wa Uhuru 2024 umepanda miti na kuifikia miradi nane ya maendeleo kwa kuitembelea, kukagua uendelevu, kuweka jiwe la msingi na uzinduzi,
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.