• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

KIKAO CHA MKOA CHA TATHIMINI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA CHF

Imewekwa tarehe: February 22nd, 2018

Kikao cha Mkoa cha Tathimini ya utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwa robo mwaka ya kuanzia mwezi Oktoba mpaka Disemba, kimefanyika Wilayani Pangani tarehe 22/02/2018.

Kikao hicho kilichoandaliwa na kufanyika kwa ufadhili wa shirika la GIZ Mkoa wa Tanga kimehudhuriwa na washiriki mbalimbali wakiwemo wahe. Wakuu wa Wilaya, wahe. Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Jiji, Miji na Halmashauri, Waganga wakuu wa Halmashauri, Maafisa Mipango na Waratibu wa CHF. Pia kikao hicho kilihudhuriwa na wawakilishi wa mashirika mbalimbali yanayotoa huduma za Afya kwa jamii kwa kushirikiana na Serikali (PPP) likiwemo shirika la CSSC. Wawakilishi wa MSD, NHIF na Wizara ya Afya pia walikuwepo.

Baada ya kuona tathimini ya hali ya Utekelezaji wa shughuli za CHF na maoni mbalimbali kutoka kwa washiriki, mgeni Rasmi na Mwenyekiti wa kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tanga mhe. Martin Shigella aliwapongeza washiriki wote kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuwataka waongeze nguvu katika kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa CHF kwani ni rahisi kwa mwananchi aliyejiunga na Mfuko wa CHF kupata huduma za Afya kuliko yule ambaye hajajiunga. Pia aliwaomba kutafuta namna nzuri ya kuwaangalia wazee na walemavu kwa kuwakatia kadi za CHF ili nao wapate huduma za Afya kwa urahisi bila usumbufu wowote.  Mhe. Mkuu wa Mkoa amewaagiza Wakurugenzi kuhakikisha wanaidhinisha na kusimamia pesa za miradi kwa wakati ili kuepuka fedha hizo kubaki wakati wananchi wanahitaji huduma bora.

 Awali ya hapo waratibu wa CHF kutoka kila Halmashauri walitoa taarifa fupi kuhusu mwenendo na utekelezaji wa shughuli za CHF katika maeneo yao. Mratibu wa CHF Mkoa alihitimisha kwa kuonyesha hali halisi ya Utekelezaji wa CHF hadi Disemba 2017, ambapo alionyesha kuwa:-

      (i) Robo ya Julai - Septemba 2017 kulikuwa na jumla ya kaya 259,751 (63%)  zilizojiunga na mfuko wa afya ya Jamii (CHF).

      (ii) Robo ya Oktoba - Disemba 2017 jumla ya kaya 290,377 (70%) zimejiunga na mfuko wa Afya Jamii (CHF).

      (iii) Jumla ya kaya 30,626 (7.4%) zimeongezeka kupitia Halmashauri zetu.

      (iv) Ongezeko kubwa katika robo hii (Oktoba - Disemba 2017) limetokana na malipo ya KWF yaliyolipwa kwa ajili ya wategemezi wa akina mama 47,294 ambazo ni Jumla ya Tshs. 526,240,000.

Pamoja na ufadhili wa vikao vya kila robo mwaka, GIZ wamekuwa wakiziwezesha Halmashauri za Mkoa wa Tanga vitendea kazi kama vile Kompyuta, Printer, friji na Stoo za dawa.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RAS MCHATTA: SINA MANENO MENGI, NIPIMENI KWA KAZI, UWAJIBIKAJI

    June 30, 2025
  • BALOZI BATILDA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIKILIZA KERO, AWAAPISHI WAWILI TANGA

    June 30, 2025
  • RC BATILDA ATAKA MAADILI, UTAWALA BORA KUIMARISHWA SERIKALINI

    June 25, 2025
  • MIAKA MINNE, SIKU 23 ZA RAS MNYEMA TANGA, AHAMISHIWA PWANI

    June 24, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.