• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MZUMBE KUKUZA UJUZI UNAOKIDHI RASILIMALI ZA KIUCHUMI

Imewekwa tarehe: February 16th, 2026

Na Mashaka Mgeta, MKINGA


CHUO Kikuu cha Mzumbe kimetangaza kuwekeza zaidi kwenye programu za kukuza ujuzi kwa vijana wanataaluma, ili kukidhi uendelezaji rasilimali zilizopo kwenye maeneo mbalimbali nchini.


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,  Profesa Daniel Mushi ameyasema hayo alipozungumza kwenye hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Kampasi ya Tanga ya Chuo hicho iliyopo wilayani Mkinga.


Hafla ya uwekaji jiwe la msingi imehudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali serikalini na taasisi binafsi, na wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Mhe Dkt Mwigulu Nchemba.


Profesa Mushi ametoa mfano kuwa azma hiyo itatekelezwa kwenye Kampasi ya Mkinga ambayo miongoni mwa maeneo ya ujuzi yatakayotiliwa mkazo katika ufundishaji ni kuhusu matumizi na uendelezaji wa rasilimali za baharini.


Mradi wa Kampasi ya Tanga ya Chuo Kikuu cha Mzumbe unaogharimu Shilingi 16,015,580,000 unajengwa kwa ushirikiano wa Serikali na Benki ya Dunia (WB).


Profesa Mushi amesema chuo hicho kinachotarajiwa kudahili wanafunzi kwa kipindi cha masomo kianzia Oktoba mwaka huu, kitawalenga wanafunzi waliomaliza kidato cha sita na waliomaliza kidato cha nne watakaoanzia ngazi ya stashahada.


Amesema, Mzumbe inatambua ongezeko la vijana wanaohitimu vidato vya nne na sita, hasa baada ya mafanikio makubwa ya utoaji elimu ya msingi bila malipo.


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amesema ujenzi wa Kampasi hiyo ni mwendelezo uboreshaji sekta elimu ambapo kwa mwaka 2025/2026, mkoa huo ulipokea Shilingi bilioni 359.


Anasema fedha hizo zilitolewa kwa ujenzi wa miundombinu kama shule mpya za msingi na sekondari, Vyuo vya Ufundi Stadi (VETA), miongoni mwa mingine.


Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Mzumbe, Profesa Saida Yahya-aothman amesema uwepo wa Kampasi hiyo wikayani Mkinga, unatokana na uhakika wa mazingira bora kwa kufundisha, kujifunza na kushiriki elimu ya vitendo, kwa kuzingatia mahitaji ya soko la ajira.


Hata hivyo, Profesa Saida amesema chuo hicho kinahitaji kufikishiwa huduma muhimu kama vile  maji, umeme ili kusiwepo kikwazo wakati wa kuanza mwaka wa masomo utakapoanza.


Waziri Mkuu, Mhe Dkt Mwigulu, amezielekeza Wizara ya Nishati, Wizara ya Maji na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kuhakikisha huduma hizo zinafikishwa chuoni hapo kabla ya Oktoba, mwaka huu.


Amesema, uwekezaji wa Chuo hicho ni miongoni mwa miradi inayoiheshimisha nchi, na kuwa ishara halisi ya dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwatumikia wananchi.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MZUMBE KUKUZA UJUZI UNAOKIDHI RASILIMALI ZA KIUCHUMI

    February 16, 2026
  • MWIGULU ASEMA: NINASAFISHA 'VICHAKA VYA UBADHIRIFU' WA MALI ZA UMMA

    February 15, 2026
  • AWESO, MHANDO WAPIGA MAGOTI KUOMBA BARABARA YA LAMI TANGA

    February 15, 2026
  • AWESO, MHANDO WAPIGA MAGOTI KUOMBA BARABARA YA LAMI TANGA

    February 15, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.