Shughuli za uchumi na uzalishaji zinazotekelezwa na Wananchi wa Mkoa wa Tanga zipo kwenye maeneo mbalimbali ya sekta ya kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili na utalii. Aidha, shughuli nyingine za uzalishaji zinazotokana na ukuzaji wa viwanda, biashara na uwekezaji unaozingatia ujasiliamali katika sekta za umma na binafsi.
Wananchi zaidi ya asilimia 80 wamejikita katika shughuli za kilimo na wanaoishi maeneo ya mwambao wa bahari ya Hindi wanajishughulisha na uvuvi mdogo mdogo. Shughuli hizi za kiuchumi na uzalishaji zimepelekea pato la mwananchi wa Tanga kuongezeka kutoka shilingi 1,936,701 mwaka 2015 hadi shilingi 2,591,074 mwaka 2018 na hii iliwezesha Mkoa kuchangia pato la Taifa kwa asilimia 4.65