Sekta ya maji imeweka mikakati ya kupunguza kero ya upatikanaji wa maji safi na usafi wa mazingira kwa kuboresha huduma ya upatikanaji wa maji safi kutoka wastani wa asilimia 61 hadi 90 na usafi wa mazingira kutoka wastani wa asilimia 75 kwenda 100. Hata hivyo imeweza kupunguza kero ya upatikanaji maji kwa wananchi wa Tanga zaidi ya asilimia 57.2 kwa kupata huduma hii chini ya umbali wa mita 400.
Wakazi wa vijijini 1,006,775 kati ya 1,864,361 sawa na asilimia 54 wamepata huduma ya maji. Wakazi wa jiji la Tanga 189,747, kati ya 213,199 sawa na asilimia 89 wanapata huduma ya maji, na wakazi wa Miji Mikuu ya Wilaya na Mji Mdogo wa Mombo 94,282 kati ya 181,199 sawa na asilimia 52 wanapata pia huduma ya maji.
Mkoa una miradi mikubwa miwili inayosimamiwa na Mamlaka ya Kitaifa Handeni Trunk Main na mradi wa maji wa Jiji la Tanga unaosimamiwa na Mamlaka ya Maji na Mazingira (TANGA UWASA). Zipo pia mamlaka za mji zilizopo miji mikuu ya wilaya zinazotoa huduma kulingana na Sheria zilizopo ikiwemo Sheria namba 5 ya mwaka 2019. Miradi 4869 yenye jumla ya vituo 5369 vya kuchotea maji vinahudumia watu katika maeneo ya vijiji katika Mkoa wa Tanga na inasimamiwa na RUWASA ngazi ya wilaya kwa kushirikiana na jumuia za watumia maji katika ngazi ya vijiji.
Kufikia Desemba 2019 jumla ya miradi 51 yenye gharamaza Sh. bilion 26,377,712,131 imekwishakamilika, miradi hiyo iko katika wilaya za Lushoto, Mkinga, Muheza, Pangani, Tanga , Handeni, Kilindi na Korogwe na miradi 28 yenye gharama za Sh. Billion 26,920,062,619.16 inaendelea kutekelezwa katika wilaya mbalimbali yenye uwezo wa kuhudumia watu wapato 197,073 baada ya kukamilika kwake.