• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MAAFISA BIASHARA TANGA 'WAJIFUNGIA' KUJADILI UWEKEZAJI, VIWANDA

Imewekwa tarehe: October 3rd, 2025

Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA

TAKRIBANI siku 215 tangu Mhe Rais Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, atangaze azma ya kuiresha Tanga ya Viwanda, Maafisa Biashara na Uwekezaji wa Halmashauri za mkoa huo, ‘wamejifungia’ kwa siku mbili kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kujadili namna bora zaidi ya kuboresha uwekezaji mkoani humo.

 Februari 28, 2025, Mhe Rais Dkt Samia alihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ambapo pamoja na mambo mengine, alisisitiza azma ya Serikali kuvifufua viwanda vuilivyokufa na kufanikisha uanzishwaji wa viwanda vipya mkoani Tanga.

Baada ya agizo hilo, mamlaka tofauti hususani Ofisi ya Mkuu wa Tanga kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara na sekta binafsi, zimeshiriki jitihada za kufanikisha utekelezaji wa azma hiyo.

Katika utekelezaji huo, Maafisa Biashara na Uwekezaji kutoka halmashauri 11 za Tanga, wamekutana kuanzia Oktoba 2 hadi 3, mwaka huu kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, wakijadili kwa kina maarifa, mbinu na stadi zinazohusu maeneo tofauti ya kuinua uwekezaji mkoani humo.

Akifungua kikao hicho, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Rashid Mchatta, amewataja Maafisa hao kama kada yenye kukutana na Kundi kubwa la wafanyabiashara na wawekezaji, hivyo kuwahimiza umuhimu wao katika kuweka na kuwezesha mazingira bora kwa wadau hao wa maendeleo.

Kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Tawala Mkoa Msaidizi (Mipango na Uratibu), Amina Kibunde, Katibu Tawala Mkoa huyo amesema, kikao hicho ni sehemu ya azma ya Serikali kuifungua Tanga kupitia uwekezaji na washiriki kujadili mazingira wezeshi na rafiki kwa sekta hiyo.

Pia amesema, miongoni mwa maeneo ya kujadiliwa kwenye kikao hicho ni pamoja na masuala ya sheria, kanuni na taratibu zinazohusiana na uwekezaji.

“Kikao hicho ni muhimu kwa wataalamu hao wa uwezeshaji, viwanda na biashara kuhudumia kundi kubwa la wafanyabiashara na wawekezaji  katika maeneo yao, kuelezana namna bora ya kudumisha ustawi wa uwekezaji ili kuongeza kipato cha mkoa na taifa kwa ujumla,” amesema.

Kupitia hotuba hiyo, Mchatta amesema wadau wa uwekezaji wanapaswa kuendeleza ushirikiano na kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara na wawekezaji kwa ujumla.

Naye Afisa Mhamasishaji kutoka Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Cuthbert Kangila, pamoja na mambo mengine, ametaja sehemu ya viashiria vya mazingira bora kwa uwekezaji Tanga kuwa ni ardhi yenye rutuba na ukubwa wa hekta 1,893,000 ambapo kati ya hizo, hekta 686,500 zinazofaa kwa kilimo hazijatumika.

Kangila amesema, uwepo wa bandari iliyoboreshwa, ni fursa nzuri ya usafiri na usafirishaji bidhaa kwenda ama kutoka kwenye masoko ya kikanda na kimataifa huku kukiwa na uhakika wa umeme wenye ziada ya jumla ya Megawati 41 kwenye halmashauri zote 11 kupitia gridi ya Taifa.

Pia, amesema Tanga ina mtandao wa barabara zenye urefu wa jumla ya kilomita 8,409 zinazouunganisha mkoa huo na barabara kuu za kikanda wakati uwepo wa vijana wanaokadiriwa kuwa milioni 2.6 unatoa uhakika wa nguvu kazi kwa uzalishaji.

Kangila amezitaja fursa nyingine zilizopo kwa wingi mkoani Tanga kuwa ni kwa sekta za uvuvi, misitu, madini na utalii.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • GCUs WATAKIWA KUTUMIA HABARI KUCHAGIZA TABASAMU KWA WATANZANIA

    November 21, 2025
  • BALOZI BATILDA AWAONGOZA MAELFU KUPIGA KURA TANGA

    October 29, 2025
  • MAAFISA BIASHARA TANGA 'WAJIFUNGIA' KUJADILI UWEKEZAJI, VIWANDA

    October 03, 2025
  • MAAFISA BIASHARA TANGA 'WAJIFUNGIA' KUJADILI UWEKEZAJI, VIWANDA

    October 03, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.