Tunampongeza Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Joseph Magufuli kwa kuendelea kuboresha na kutekeleza mpango wa utoaji elimu bila malipo. Kuanzia kuanza kwa Mpango huu Mkoa umepokea kiasi cha shilingi 49,587,684,178.20 (bilioni49.6) kama ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi na sekondari na posho ya madaraka.
Hadi kufikia Disemba 2019, Mkoa umepokea kiasi cha shilingi 13,113,302,816.42 (bilioni 13.1) kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu na ukarabati wa shule kongwe za Usagara, Korogwe girls, Tanga Tech na Mkwakwani.
Uandikishaji wa wanafunzi katika ngazi zote umeongezeka kuanzia mwaka 2015 hadi 2019. Awali mwaka 2015 walioandikishwa walikuwa 64,153 ukilinganisha na mwaka 2019 waliandikishwa wanafunzi 71,306 sawa na ongezeko la asilimia 11.1. Uandikishaji wa darasa la kwanza mwaka 2015 waliandikishwa wanafunzi 65,000 ukilinganisha na mwaka 2019 walioandikishwa walikuwa wanafunzi 67,524 sawa na ongezeko la asilimia 3.8.
Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga Kidato cha kwanza mwaka 2015 walikuwa 26,261 ukilinganisha na mwaka 2019 walikuwa 35,728 sawa na asilimia 36.05. Hali hii ya ongezeko inatokana na utekelezaji wa mpango wa utoaji elimu bila malipo.Wazazi wengi wamepeleka watoto wao shule.
Ufaulu katika Mkoa kwa upimaji wa darasa la nne kwa mwaka 2019 ulikuwa waasilimia 91.35 sawa na upungufu wa asilimia 2.14 kutoka asilimia 96.50 za mwaka 2018. Matokeo ya Mtihani wa kumaliza darasa la saba ufaulu ulikuwa wa asilimia 76.44 kutoka asilimia 72.7 ya mwaka 2018 sawa na ongezeko la asilimia 3.74. Matokeo ya upimaji wa kidato cha pili ufaulu ulikuwa ni asilimia 86.04 kwa mwaka 2019 ambapo ni upungufu wa asilimia 0.45 kutoka asilimia 86.49 ya mwaka 2018.
Aidha, matokeo ya mitihani ya kumaliza kidato cha nne ufaulu ulikuwa wa asilimia 72.97 kwa mwaka 2019 sawa na upungufu wa asilimia 1.45 kutoka asilimia 74.42 za mwaka 2018.