HOSPITALI ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga (Bombo), imezindua Wodi Binafsi inayoongeza juhudi za kuboresha utoaji wa huduma bora za afya kwa wakazi wa mkoa huo na maeneo ya jirani.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Rashid Mchatta (pichani aliyevaa tai katikati), aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amesema wodi hiyo ni sehemu ya ishara za dhamira ya Serikali, kuboresha huduma za afya nchini.
“Huduma hii inaakisi dhamira ya Serikali katika utoaji huduma bora na za viwango vya juu kwa wananchi. Pia inakuza huduma za tiba utalii kwa miji inayopakana na nchi yetu,” amesema Mchatta.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Bombo, Dkt Frank Shega, amesema wodi hiyo ina uwezo wa kuwahudumia wagonjwa 10 kwa wakati mmoja.
Kwa mujibu Dkt Shega, wodi hiyo imejengwa kwa muundo unaojumuisha vyumba vya kulala wagonjwa wawili, chumba cha mgonjwa mmoja na chumba cha watu maarufu (VIP), vyote vikiwa na huduma muhimu ikiwemo lishe na uangalizi wa kitaalamu.
Naye Mwakilishi wa Wizara ya Afya kutoka Idara ya Rasilimali Watu na Utawala, Grace Sheshui, amepongeza uongozi wa Bombo kwa kuanzisha wodi binafsi, kwamba inachangia kuinua ubora wa huduma kwa wakazi wa Tanga.
Uzinduzi wa wodi hiyo unatarajiwa kuongeza chaguo la huduma bora kwa wananchi, kupunguza msongamano katika wodi za kawaida na kuchochea ukuaji wa huduma rafiki kwa wagonjwa kutoka ndani na nje ya nchi.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.