EACOP YAELEZA MAENDELEO YA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amekutana na timu ya Mahusiano na Jamii kutoka Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi Afrika Mashariki (EACOP), kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya utekelezaji wa mradi huo.
Timu hiyo iliwasilisha hatua za utekelezaji wa mradi na kumtambulisha mkandarasi kutoka kampuni ya Sheria Kiganjani, atakayesimamia mradi wa kuwawezesha vijana kiuchumi katika wilaya za Tanga, Muheza na Korogwe.
Wanufaika wakuu wa mradi huo ni vijana 679 waliopo kwenye vikundi, na wenye ujuzi wa fani mbalimbali watakaondelezwa kupitia VETA na SIDO. Katika utekelezaji wa mradi huo ambapo hadi sasa , wamepatikana vijana 560.
Afisa Mahusiano ya Jamii wa EACOP, Daniel Semkiwa, amesema utekelezaji unaendelea vizuri ukihusisha ujenzi wa matenki uliofikia asilimia 85, kazi ya jet imefikia asilimia 84 na ujenzi wa terminal asilimia 45.
Aidha, amesema EACOP inaendelea kutekeleza mradi wa Uboreshaji Maisha ya Waguswa (MKUBA) katika maeneo ya Chongoleani na Putin, ambapo jumla ya vikundi 16 vimeundwa na vitapewa Shilingi milioni 33.6 kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.