• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MWIGULU ASEMA: NINASAFISHA 'VICHAKA VYA UBADHIRIFU' WA MALI ZA UMMA

Imewekwa tarehe: February 15th, 2026


Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA


DHANA ya 'fekeo na rato' vinavyoashiria utayari wa Waziri Mkuu, Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba kuchochea utendaji kazi bora serikalini, uwajibikaji na  udhibiti ubadhirifu wa mali ya umma, inaonekana kwa vitendo.


Akiwa katika ziara yake mkoani Tanga kuanzia Februari 13, 2026, Mhe Dkt. Mwigulu, anasema pamoja na kutembelea, kukagua, kuweka mawe ya msingi ama kufungua miradi ya maendeleo, pia anashughulikia 'mambo yanayokwama' kwenye miradi ya maendeleo, huduma za ustawi na sababu za mkwamo husika.


Anasema, sehemu ya mikwamo hiyo inatokana na sababu zinazotumika kama 'vichaka vya ubadhirifu wa mali ya umma', vinavyofanywa na watumishi wa umma wasiokuwa waadilifu, wanaoichafua Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.


Mathalani, akiwa wilayani Handeni, Mhe Dkt Mwigulu alibaini kuwepo milango 34 isiyokuwa na ubora, iliyowekwa kwenye Kituo cha Afya na kuganda kwa mifuko 1,262 ya saruji iliyotakiwa kutumika kwenye ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) wilayani Handeni.


Pia, Mhe Dkt Mwigulu amebaini kuwepo mkandarasi Hamimu Kusaga wa kampuni ya Green Construction iliyoshinda zabuni ya mradi wa ukarabati na upanuzi katika Mji Mdogo Mombo wilayani Korogwe, kuondoka na fedha alizolipwa huku akiutekeleza mradi huo wenye thamani ya Shilingi  xxxx


Mhe Dkt Mwigulu ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi wa kina na haraka kwenye maeneo hayo, na kumpatia taarifa ikihusisha majina ya wahusika,  kwa hatua zaidi.


Amesema, kwa mradi wa VETA ulio chini ya usimamizi wa Wizara ya Elimu, Katibu Mkuu wa wizara hiyo awachukulie hatua wahusika, ikiwa ni pamoja na kuwakata mishahara yao ili fedha hizo zitumike kununua saruji iliyoganda.


"Nikiyafanya haya watu wanasema nimekuwa mkali na kwamba nitachukiwa, sijaja hapa kupendwa, nipo hapa kusafisha vichaka vya ubadhirifu na wizi wa mali za umma," anasema.


Mhe Dkt Mwigulu anasema, kuna ishara za wazi kuwepo mbinu kwa watumishi wasiokuwa waaminifu, kutumia mifumo yenye kuhalalisha ukubwa wa gharama hasa kwenye ujenzi wa miundombinu mbalimbali, ili kujinufaisha.


Anaonya, "fedha za umma ni za kuogopa, usidhani ni kama matunda pori kila anayepita anachuma...ninawaonya watumishi na wadau wetu katika sekta binafsi, msihiriki ubadhirifu ama wizi wa mali ya umma," anasema.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • MZUMBE KUKUZA UJUZI UNAOKIDHI RASILIMALI ZA KIUCHUMI

    February 16, 2026
  • MWIGULU ASEMA: NINASAFISHA 'VICHAKA VYA UBADHIRIFU' WA MALI ZA UMMA

    February 15, 2026
  • AWESO, MHANDO WAPIGA MAGOTI KUOMBA BARABARA YA LAMI TANGA

    February 15, 2026
  • AWESO, MHANDO WAPIGA MAGOTI KUOMBA BARABARA YA LAMI TANGA

    February 15, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.