DONDOO ZA MWENGE WA UHURU
WAZO la kukimbiza Mwenge wa Uhuru nchi nzima na kila mwaka lilitolewa na vijana wa TANU katika kikao chao kilichofanyika tarehe 26 Juni, 1964.
(Baadaye yaani Februari 5, 1977, TANU ambayo kirefu chake ni Tanganyika African National Union) kiliungana na Afro Shiraz Party (ASP) cha Zanzibar, kikazaliwa Chama Cha Mapinduzi - CCM)
Lengo kuu likiwa ni kutekeleza kwa vitendo azma ya Baba wa Taifa ya kuhamasisha umoja, upendo, amani na ujenzi wa Taifa kwa kuhamasisha maendeleo.
Tangu wakati huo, Mwenge umekuwa ukikimbizwa katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kupitia mbio hizo hamasa kubwa imetolewa ili kuendelea kudumisha amani, na kujenga uzalendo, umoja na mshikamano.
Katika kipindi chote hicho, mbio za Mwenge zimekuwa na mafanikio makubwa yanayosadifu maono ya waasisi wa Taifa letu.
Chanzo: Hotuba ya Makamu wa Rais, Mhe Dkt Philip Isdor Mpango kwenye sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2025.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.