Na Mashaka Mgeta, MKINGA
NAIBU Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati, Mhe Dk Doto Biteko, ameziagiza halmashauri za majiji, manispaa, miji na wilaya nchini kugharamia miradi midogo inayojibu kero za wananchi kwenye miradi mikubwa ya maendeleo nchini.
Mhe Dk Biteko ametoa agizo hilo leo mjini Tanga, wakati akizindua kwa kuwasha umeme kwenye vijiji vya Magodi na Kigandini wilaya ya Mkinga mkoani Tanga, unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) na Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Mhe Dk Biteko amesema yapo mahitaji yanayoibuka baada ya kukamilika kwa miradi mikubwa inayogharamiwa na Serikali Kuu, yanayoweza kupatikana kwa gharama za halmashauri, lakini hali inakuwa sivyo.
Alikuwa akizungumzia uhitaji wa kisima kwenye zahati ya kijiji zahati ya kijiji cha Magodi iliyonufaika kwa umeme wa REA, lakini inahitaji kisima cha maji kwa matumizi yake.
Mhe Dk Biteko amesema wakati wilaya hiyo ikisubiri kukamilika kwa mradi wa maji kutoka Mto Zigi, halmashauri ya wilaya ya Mkinga ihakikishe kisima hicho kinajengwa na kukamilika ifikapo Machi mwaka huu.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.