SERIKALI mkoani Tanga imepokea jumla ya madarasa mapya 77 yaliyojengwa na Halmashauri ya Wilaya na ya Mji Handeni yenye thamani ya Shs. Bilioni 1.540 ambapo ujenzi wake umekamilika wiki mbili kabla ya muda uliyopangwa tarehe 15 Desemba 2022.
Madarasa hayo yatawawezesha wanafunzi wapya zaidi 8000 wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza 2023 waweze kuanza masomo yao.
Akizungumza na viongozi wa Wilaya hiyo katika Shule ya Sekondari Mkata, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba mara baada ya kuikagua shule hiyo na kuzindua Shule hizo ameipongeza Wilaya hiyo kukamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa wakati kabla ya muda uliotangazwa na TAMISEMI wa Desemba 15 mwaka 2022.
Amesema baada ya kufuatilia ujenzi huo Wilayani hapo ameridhika na ujenzi wa viwango, uliyokamilika kwa muda muaafaka na kwa thamani ya fedha.
" Hongera sana Mkuu wa Wilaya ya Handeni Seriel Mchembe kwa kuwa wa kwanza kukabidhi madarasa mapya na nataka Halmashauri nyingine kuiga mfano huo pamoja na kubakisha chenji kuongeza sehemu ya ofisi ya walimu na vyoo" akisisitiza zaidi.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Handeni Siriel Nchembe amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa kiasi hicho cha fedha ambazo zimekamilisha ujenzi wote wa vyumba vya madarasa kwa wakati.
Aidha ametaja siri ya Wilaya kuwa wa kwanza kukabidhi madarasa kwa wakati, ni ushirikiano uliofanywa na viongozi wa Wilaya hasa Maafisa Watendaji na Tarafa.
"Nashukuru Mkuu wa Mkoa wa Tanga ushauri wake tuliufanyia kazi na ndio tukawapa madaraka maalum maafisa watendaji na Tarafa ndio haya matokeo ya kazi kukamilika kabla ya wakati na viwango hadi tailes madarasani"
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.