ZIARA YA DK BITEKO KUWASHA UMEME TANGA
Na Zuberi Mgaya,MUM-TANGA
NI ziara inayoviingiza vijiji viwili vya Magodi na Kigandini kuifanya idadi ya vijiji 82 kati ya 85 vilivyopo wilayani Mkinga mkoa wa Tanga kuwa na umeme.
Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Nishati Mhe Dk Doto Biteko, amefanya ziara ya siku tatu inayomfikisha wilayani Mkinga na kuwasha umeme uliowekwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) kwenye vijiji hivyo viwili ambavyo awali, havikuwa na huduma hiyo.
Hafla ya kuwasha umeme imefanyika kwenye zahanati ya kijiji cha Magodi na nyumba ya mkazi wa kijiji cha Kigandini, Mwanaisha Salehe.
Wilaya ya Mkinga, imeshapokea miradi ya umeme wa REA kwenye vijiji 82 kati ya 85 vilivyopo wilayani humo vyenye thamani ya Shilingi bilioni 8.23.
Pia, Dk Biteko ameahidi kutatua kero ya barabara inayotoka tarafa ya Maramba kwenda halmashauri ya wilaya ya Mkinga ambayo kwa mujibu wa Mbunge wa Mkinga, Mhe Dustan Kitandula, imetajwa kwenye Ilani ya CCM ya 2020 – 2025.
Naye Mwakilishi wa TANESCO mkoa wa Tanga, Jones Zolutu amesema ofisi yake imeandaa mipango ya kusambaza umeme ikiwemo kwenye maeneo ya kipaumbele kwenye jamii kama viwanda na vituo vya kutolewa huduma za afya.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.