Na Mwandishi Wetu, KILINDI
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Lucy Kabyemera amewataka wakazi wa wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, kuheshimu mpango wa matumizi Bora ya ardhi ili kuepuka migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao.
Kabyemera ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye kijiji cha Mswaki wilayani Kilindi, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga kuanzia Februari 23 hadi Machi 1, 2025.
Akiwa kwenye ziara hiyo, pamoja na mambo mengine, Mhe Rais Dkt Samia, alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe Deogratius Ndejembi, kuifikisha huduma ya kliniki ya ardhi wilaya Kilindi, ikiwa ni njia muafaka ya kupatikana suluhu ya kudumu ya migogoro ya ardhi hasa kati ya wakulima na wafugaji.
Kliniki ya ardhi imefanyika kwenye kijiji cha Mswaki ambapo Kabyemera amesema, Wizara hiyo itatuma timu ya wataalamu wilayani humo, kuhakikisha maeneo ambayo hayapangwa kwa matumizi bora ya ardhi, yapangwe.
Kabyemera, amewahimiza wananchi wilayani humo kutumia ardhi kama ilivyopangwa, ili waishi kwa amani na kuendelea na shughuli za maendeleo.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.