• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

AWESO 'AJITISHWA' MZIGO' WA MAJI KUTIRIRIKA HANDENI

Imewekwa tarehe: February 14th, 2026

Na Mashaka Mgeta, HANDENI

AHADI ya Mbunge wa Handeni Mjini, Mhe Reuben Kwagilwa, kuoga hadharani pindi maji yanayotokana na uboreshwaji wa miundombinu ya mradi wa maji wa Handeni Truck Main (HTM) yatakapotoka, inamuibua Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso.

Mhe Kwagilwa ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali (TAMISEMI), mbele ya Waziri Mkuu, Mhe Dkt Mwigulu Nchemba, akairejea ahadi ya kuoga hadharani akiwa amevaa nguo, kuashiria furaha ya kupatikana maji yaliyo miongoni mwa kero zilizodumu muda mrefu wilayani Handeni.

Kauli ya Mhe Kwagilwa inakuwa sababu kwa Mhe Aweso, kutoa ufafanuzi wa hoja hiyo na nyingine zilizoibuliwa na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mhe Mwigulu kwenye uwanja wa Handeni Square.

Mhe Aweso, anathibitisha kuwepo kero ya maji Handeni na kusema zipo hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuondokana na kadhia hiyo.

Kwa mujibu wa Mhe Aweso, hatua hizo ni pamoja na utekelezaji wa mradi wa HTM unaolenga kubadilisha miundombinu kutoka iliyokuwa tangu mwaka 1974 na kuweka ya kisasa, kupitia mradi unaogharimu Shilingi bilioni 171.

Mhe Aweso, kama vile ‘amejitwisha mzigo’ wa dhamana kwa wakazi wa Handeni, anasema mradi huo utakamilika muda mfupi ujao, na baada ya Bunge litakalofanya mkutano na vikao vyake kuanzia mwishoni mwa Machi mwaka huu, mradi huo utazinduliwa na hivyo kuyafanya maji ‘yatiririke’ wilayani Handeni kwa muda wote.

Ahadi hiyo inaibua shangwe na nderemo kwa wakazi wa mji huo, wakirejea kauli ya awali ya Mhe Aweso kwamba, wakati maeneo mengine yana shida ya maji, Handeni kuna dhiki ya maji.

Mhe Aweso amesema pamoja na hatua hiyo, zipo juhudi za Serikali kujenga mabwawa kwenye maeneo ya Kibaya, Nkale, Kweingoma, Kwa Msangazi na Msasa, ili kuondokana na kadhia hiyo.Waziri wa Kilimo, Mhe Daniel Chongolo, akasema uhakika wa maji kwa jamii, ni sehemu muhimu inayovutia uwekezaji na viwanda, huku ikichagiza upatikanaji chakula cha mifugo kwenye nyanda za malisho.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • AWESO 'AJITISHWA' MZIGO' WA MAJI KUTIRIRIKA HANDENI

    February 14, 2026
  • MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUPOZA UMEME HANDENI,KILINDI

    February 14, 2026
  • MWIGULU: TUSITENGENEZE UFA WA UADUI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

    February 13, 2026
  • BALOZI BATILDA: TANGA KUZIZIMA DKT MWIGULU AKIWASILI KESHO

    February 12, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.