• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MWIGULU: TUSITENGENEZE UFA WA UADUI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Imewekwa tarehe: February 13th, 2026


Na Mashaka Mgeta, HANDENI

WAZIRI Mkuu, Mhe Dkt. Mwigulu Nchembe, ameionya jamii kuepuka vitendo na kauli zinazotengeneza na kukuza ufa wa uadui kupitia migororo ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.

Mhe Dkt. Mwigulu, ameyasema hayo leo Februari 13, 2026, alipozugumza baada ya kusikiliza kero za wananchi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye Kituo cha Kupooza Umeme kilichopo Mkata wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Alikuwa akijibu swali na mkazi wa Kijiji cha Mkata Mashariki, Omar Athuman, aliyetaka kujua mpango wa Serikali kudhibiti migogoro kati ya jamii hizo zinazoathiri mali na maisha ya watu.

Mhe Dkt. Mwingulu amesema, kwa nyakati tofauti, kuna makosa yanayomhusisha mtu mmoja, mathalani mfugaji, lakini yanakuzwa na kuwajumuisha wafugaji wote isivyo sawa.

Amesema, kama kuna mfugaji ama mkulima anatenda kosa, inastahili tafsiri ya kadhia hiyo ‘imlenge’ mhusika na hatua kuchukuliwa dhidi yake badala ya kuelekezwa kwa jamii nzima.

Pia, Mhe Dkt Mwigulu ameasa wananchi kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zinazojenga msingi wa uhuru wa kila raia kuishi mahali popote, ili kuepuka migogoro kama inayotokea kati ya wakulima na wafugaji.

“Tunaruhusiwa kuishi mahali popote lakini lazima tufuate Sheria, Kanuni na Taratibu ili kuepuka jeuri na kiburi vinavyosababisha uchokozi kama wa wafugaji kulisha mifugo kwenye mazao ya wakulima,” amesema.

Mh. Dkt Mwigulu, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian na Kamati ya Usalama (KU) ya Mkoa huo, ‘kutowafumbia macho’ watu wanaovunja sheria,  kwa vile, kutofanya hivyo kutahatarisha amani kwa watu na taifa.

Waziri wa Kilimo, Mhe Daniel Chongolo, amesema Serikali inatekeleza mipango yenye lengo la kuboresha na kuweka suluhu ya kudumu katika kudhibiti migogoro ya wafugaji na wakulima.

Amesema, miongoni mwa yanayotekelezwa kwenye mipango hiyo ni matumizi bora ya ardhi ambapo pamoja na mambo mengine, unatenganisha maeneo ya kilimo na ufugaji.

Nyingine ni matumizi ya daftari la makazi maeneo ya vijiji, litakalowezesha kuwatambua wakazi halali, hivyo kuwadhibiti wavamizi kwenye maeneo wasiyotakiwa.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • AWESO 'AJITISHWA' MZIGO' WA MAJI KUTIRIRIKA HANDENI

    February 14, 2026
  • MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUPOZA UMEME HANDENI,KILINDI

    February 14, 2026
  • MWIGULU: TUSITENGENEZE UFA WA UADUI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI

    February 13, 2026
  • BALOZI BATILDA: TANGA KUZIZIMA DKT MWIGULU AKIWASILI KESHO

    February 12, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.