Na Emma Kigombe, OMM Tanga
MKOA wa Tanga umetenga maeneo maalum kwa ajili ya uwekezaji katika sekta ya viwanda na hoteli, hatua inayolenga kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
Maeneo hayo ni pamoja na Pingoni, Amboni na Mzingani, ambayo yameainishwa kuwa fursa adhimu kwa wawekezaji `kuyachangamkia’.
Akizungumza katika ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya 12 ya Biashara na Utalii yanayoendelea jijini Jiji la Tanga kuanzia Mei 28 hadi Juni 6, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian amesema mkoa huo umejipanga kikamilifu kuweka mazingira bora ya uwekezaji.
Hotuba ya Mhe Balozi Dkt Batilda, imetolewa kwa niaba yake na Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Mhe Dadi Kolimba, akisema, mkoa una maeneo mengi yenye mvuto kwa uwekezaji, hususan katika sekta ya viwanda, na kwamba juhudi zinaendelea kuboresha miundombinu ya msingi ikiwemo barabara, maji, umeme na huduma za mawasiliano.
“Tunawahamasisha wafanyabiashara, wawekezaji pamoja na taasisi za umma na binafsi kutumia maonyesho haya kama jukwaa la kujifunza, kushirikiana na kutangaza bidhaa na huduma zao,” amesema.
Serikali ya Mkoa imeahidi kuendelea kuimarisha mazingira rafiki kwa wafanyabiashara na wawekezaji ili kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.