Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
NI dhahiri kwamba hakuna ubishi kuwa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ni mbeba maono yenye tija kwa umma na kuchagiza kasi ya maendeleo nchini.
Februari 28, 2025 alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Mkwakwani, akiwa katika ziara ya siku sita mkoani Tanga, miongoni mwa kauli zake ni kurejesha hadhi ya viwanda mkoani humo.
Takribani miezi sita sasa, viwanda vinazidi kuenea kwenye maeneo tofauti yaliyotengwa kwa uwekezaji wa viwanda, kati ya hivyo, vikiwamo vinavyofufuliwa na vinavyoanzishwa upya.
Kauli ya wamiliki wa viwanda hivyo ni kuyafurahia mazingira bora ya uwekezaji, miundombinu hasa bandari na ushirikiano kutoka kwa wakazi wa Tanga, kwamba ni matunda ya ziara ya Mhe Rais Dkt Samia, dhamira, nia na utayari wake wa kuirejesha ‘Tanga ya Viwanda’.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, anafanya ziara ya kutembelea viwanda vya mkoani humo, na leo amefika viwanda vya Anjari, Tanga Cable na Usher’s.
Mkurugenzi wa Kiwanda cha Anjari, Hatim Anjari, anasema mazingira bora yakiwemo ya nishati ya umeme wa uhakika baada ya kauli ya Mhe Rais Dkt Samia, yanachochea ukuaji biashara na mtaji katika uwekezaji wao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanga Cable Industries Limited, Moiz Dossaj, amesema kutokana na kukua kwa biashara yao baada ya hamasa ya Mhe Rais Dkt Samia, sasa wamepanga kuongeza uwekezaji ukiwemo wa mashine za uzalishaji zitakazosababisha kuongeza ajira na kiwango cha uzalishaji.
Dossaj amesema uzalishaji wa bidhaa za nyaya zikiwemo za umeme, unafanyika na kupata soko la uhakika nchini, kutokana na Mhe Rais Dk Samia kuagiza manunuzi kwa miradi ya ndani kama REA, kupitia kwa wazawa.
Naye Jayesh Asher, Mkurugenzi wa Asher’s , amesema mazingira bora yenye kuvutia uwekezaji wa viwanda, yamesababisha kukua kwa uzalishaji wa bidhaa na sasa zinauzwa hadi kwenye mataifa Kenya, Malawi, Msumbuji na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Mhe Balozi Dkt Batilda, amesema lengo la ziara yake ni kuwafikia wamiliki wenye viwanda na kujadiliana kuhusu changamooto zinazowakabili, ili kuchukua hatua za mapema kuzidhibiti.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.