Na Emma Kigombe, KILINDI
WAZIRI Mkuu, Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Februari 14, 2026 ameweka jiwe la msingi kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, inayojengwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 2.64.
Kati ya fedha hizo, Shilingi bilioni 2.51 zimetolewa na Serikali Kuu, Shilingi milioni 50 ni mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi na Shilingi milioni 89.9 zimetolewa na Benki ya Dunia (WB).
Akizungumza katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi, Mhe Dkt. Nchemba amesema, ujenzi wa hospitali hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha huduma za afya nchini, na kusogeza huduma karibu na wananchi.
Hospitali hiyo inatarajiwa kupunguza adha na gharama kubwa za matibabu ambazo wananchi wa Kilindi walilazimika kuzifuata katika wilaya za jirani.
Kupatikana kwa huduma hizo ndani ya wilaya kutarahisisha upatikanaji wa matibabu kwa wakati, kupunguza vifo vinavyoweza kuzuilika, na kuongeza ustawi wa jamii kwa ujumla.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.