• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

WAZIRI MKUU AAGIZA KUKAMATWA, KUWEKWA NDANI MKANDARASI ALIYETELEKEZA MRADI KOROGWE

Imewekwa tarehe: February 15th, 2026

Na Mashaka Mgeta, KOROGWE

WAZIRI Mkuu, Mhe Dkt. Mwigulu Nchemba, ameagiza kusakwa na kuwekwa ndani Mkurugenzi wa kampuni ya Greens Construction Limited, Hamimu Kusaga, anayedaiwa kulipwa Shilingi milioni 934 za mradi wa ukarabati na upanuzi wa katika mji mdogo wa Mombo, kisha kuutelekeza.

Mhe Dkt Mwigulu amesema, mkandarasi huyo anayedaiwa kuishi jijini Dodoma atakapopatikana, anapaswa kusakwa, kukamatwa na kuwekwa ndani hadi atakaporejesha fedha hizo, kisha hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa.

Ili kufanikisha azma hiyo, Mhe Dkt. Mwigulu, amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt. Batilda Burian, kuwasiliana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe Rosemary Senyamule, ili mkandarasi huyo akamatwe na kufikishwa Korogwe kurejesha fedha alizolipwa.

“Fedha za umma si kama matunda ya porini ambayo kila mtu anapita na kuchuma na kuondoka zake...haya ndio mambo yasiyovumilika,” amesema.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhe William Mwakilima, alisema mtuhumiwa huyo alilipwa fedha hizo kwa kipindi cha takribani miaka miwili iliyopita, na mchakato wa kumfungulia mashtaka unaendelea.

Akizungumzia mradi wa maji miji 28, Mhe Dkt. Mwigulu amesema ni matokeo ya nia na dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuwatumikia Watanzania kupitia utoaji huduma kwa maendeleo na ustawi wa watu.

Mhe Dkt Mwigulu alielekeza, kutokana na matokeo ya dhamira hiyo inayoonekana pia kwenye miradi mingine nchini, watu wasimame kama ishara ya kumheshimisha Mhe Rais Dkt. Samia, ikawa hivyo.

Naye Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso, alisema mradi huo unaosimamiwa na Handeni Truck Main (HTM), utagharimu Shilingi bilioni 171 na kuwanufaisha wakazi wa wilaya za Korogwe, Muheza na Pangani.

Amesema, awali, mradi huo wenye miundombinu iliyojengwa mwaka 1974 na kuwa chakavu, ulikuwa na uwezo wa kutoa lita za ujazo milioni 4 kwa watu 180,000 ,lakini utakapokamilika utatoa lita za ujazo milioni 52 kwa siku, ukiwanufaisha watu 860,000.

Wananchi wa wilaya hizo, wamepongeza jitihada za Serikali kufanikisha mradi huo utakawaondoa kwenye kadhia ya ukosefu wa maji ya uhakika iliyokuwepo kwa miongo kadhaa sasa.

Akizunguma kwa niaba ya wenzake, Hamza Matebe, mkazi wa Gitu “tunaona kwa vitendo namna Serikali ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inavyotuletea maji, hii inakwenda kujenga historia isiyofutika kwa wilaya za Korogwe, Muheza, Handeni na Pangani.”

 

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAZIRI MKUU AAGIZA KUKAMATWA, KUWEKWA NDANI MKANDARASI ALIYETELEKEZA MRADI KOROGWE

    February 15, 2026
  • MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA WILAYA YA KILINDI

    February 14, 2026
  • AWESO 'AJITISHWA' MZIGO' WA MAJI KUTIRIRIKA HANDENI

    February 14, 2026
  • MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUPOZA UMEME HANDENI,KILINDI

    February 14, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.