Na Emma Kigombe
Waziri wa mifugo na uvuvi Abdallah Ulega amevikabidhi kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Omary Mgumba vitua vitatu atamizi vya mifugo viwili kutoka Chuo cha mifugo Buhuri na kimoja kutoka taasisi ya utafiti wa mifugo Taliri ikiwa ni jitahada ya Serikali kuwawezesha vijana kupata mafunzo kwa vitendo yatakayowawezesha kujiajjiri na kuajiri wengine.
Ulega amekabidhi vituo hivyo mara baada ya kuwasili mkoani humo tayari kwa kuanza ziara yake ya siku tatu ya kutembelea miradi ya uvuvi na mifugo katika wilaya ya Tanga, Pangani, Muheza, Handeni na Kilindi.
Akizungumza Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amesema vituo hivyo vipo mahususi kwa ajili ya kutengeneza wafugaji mahili watakaoenda kufuga kibiashara.
"Hapa tunavituo vitatu tumeviweka katika Mkoa wako wa Tanga na leo naomba nivitambulishe na kukukabidhi kwa ufuatilaji wa kimaendeleo, hivi ni vituo atamizi vya mifugo vyote vitatu vipo hapo viwili vipo Chuo cha Buhuri na kimajo kipo katika taasisi ya mifugo Taliri vituo hivi vinatengeneza wafugaji mahili wa kesho wenye mipango mikakati ya kutengeneza watu ambao watakwenda kufuga kibiashara anenepeshe apeleka sokoni mali iliyo na ubora" alisema Ulega.
Ulega ameeleza kuwa kabla ya kuanza kwa mradi huo wa kuwawezesha vijana walitoa matangazo na takribani vijana 600 walijitokeza lakini lengo la serikali lilikuwa kuwapata vijana 240 na katika Mkoa wa Tanga umetoa vijana 90.
"Huu mradi wa wizara unaohusisha mafunzo kwa vitendo namna ya kuandaa shamba (malisho) wale kazi yao tunaanza kuwaelekeza toka mwanzo hatua za uandaaji kisha uandaaji wa banda bora kwa hiyo toka siku ya kwanza anafundishwa kwa vitendo" aliongeza Ulega.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe Omary Mgumba ameishukuru Serikali kupitia wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuwekeza katika miradi mingi katika sekta hiyo na kuahidi kuisimamia kwa ukaribu ili kuyaona matokea ya uwekezaji huo.
" Huu mfumo mliouweka wa atamizi wa vijana kuwakusanya pamoja ma kukaa mwaka mzima kwa ajili ya elimu ya vitendo ni jambo kubwa sana na vijana ninauwakika baada ya kutoka pale wataweza kujiajiri wenyewe " alisema Mgumba
Pia Mgumba amesema kuwa dhamira ya Rais Dkt. Samia na Serikali yake ni kubadilisha ufugaji wa kujikimu na kwenda ufugaji wa kibiashara hivyo kupitia vituo hivyo kutasaidia vijana kubadili fikra na kujikita katika ufugaji wa biashara.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.