Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba ameridhishwa na hatua ya ujenzi wa Shule ya Wasichana Mkoa inayojengwa katika Wilaya ya Kilindi mkoani humo.
Akiwa katika ziara yake ya kukagua Ujenzi huo wa Shule amesema kuwa hadi sasa ujenzi huo ambayo umekamilika kwa asilimia 75 una simamiwa vizuri na viongozi wa Wilaya ya Kilindi kwani thamani ya pesa (value for money) inaonekana kwa kiasi kikubwa sana.
Hata hivyo amesisitiza hadi ifikapo tarehe 15 February 2024 lazima ujenzi huo uwe umekamilika.
Serikali chini ya Mhe. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi cha fedha Bilioni 3 kwa Mkoa wa Tanga kwa ajili ya Ujenzi wa Shule ya Wasichana ya Mkoa Mabalanga Wilaya ya Kilindi.
Picha na taarifa imeandikwa na Jamal Zuberi wa OMM Tanga.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.