Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amewataka viongozi mkoani hapa kuhakikisha mfumo wa anuani za makazi (Post Code) unakamilika kwa wakati ili kuwezesha serikali kuwafikia wananchi kwa haraka.
Malima amesema hayo leo Jumatano Februari 16, kabla ya kuzindua zoezi la kuhakiki nyumba na mitaa jijini hapa.
Amesema lengo la serikali ni kuhakikisha kila mtaa unafahamika na kila nyumba inakuwa na namba ili kuiwezesha serikali kufikisha huduma muhimu kama vile zimamoto na huduma nyingine muhimu kwa haraka zaidi kwa wananchi.
"Zoezi hili linatakiwa kukamilika mapema kabla ya Mei mwaka huu, hivyo basi Kamati Maalumu ya Mkoa ihakikishe suala hilo linaratibiwa na kusimamiwa ili likamillike kwa wakati," amesema RC Malima.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.