• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

RC MALIMA KUENDELEZA USHIRIKIANO NA MAHAKAMA KUTENDA HAKI KWA WANANCHI

Imewekwa tarehe: February 2nd, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Adam Malima amesema ofisi yake itaendeleza uhusiano mzuri baina yake na mahakama zote jijini humo ili kudumisha utawala wa sheria na kuwatendea haki wananchi.

Malima amesema hayo leo Jumanne Februari 2, katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mahakama jijini Tanga na kuongeza kuwa hayo yote yanawezekana kila mtu akitambua nafasi yake na kuheshimu nafasi ya mwenzake.

Aidha, Malima ambaye alikuwa mgeni maalumu katika maadhimisho hayo amewapongeza watumishi wa mahakama wakiwamo majaji na mahakimu huju akiwataka kutenda haki hususani kwa wasiokuwa na kipato.

“Binafsi nawapongeza kwa hatua mliyoanza kuchukua ya maboresho ya mahakama kuwa ya kimtandao, hii itasaidia kuleta ufanisi na kuweka uwazi lakini pia kuokoa muda na haki ikapatikana ni jambo zuri.

“Lakini kuna jambo ambalo huwa linaniumiza sana ndani ya nafsi yangu hili la upatikanaji wa haki kwa wale wenye uwezo mdogo wa kipato, nawaomba mfumo huu utusaidie watendewe haki,” amesema Malima.

Pamoja na mambo mengine, Malima amezungumzia utawala wa sheria akitolea mfano watu kujichukulia sheria mkononi katika mapigano ya wakulima na wafugaji wilayani, ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia.

“Utawala wa sheria ni watu kutojichukulia sheria mkononi na kutofanya mambo yasiyo na maslahi kwa wananchi. Kuna watu wanabaka watoto... tuwaache watoto wawe watoto na sheria iwalinde, Tanga ninayoongoza mimi hakuna nafasi hiyo,” amesema.

Awali, Jaji Mkuu wa Mkuu Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, Latifa Mansoor alisema katika wiki ya sheria ambayo kilele chake kimefikia leo mambo mbalimbali yamefanyika ikiwamo kutoa elimu ya sheria kwa wadau na wananchi magerezani, mashuleni na kwenye viwanja vya wazi huku akisema wananchi wote ni wanasheria.

“Kuna wanasheria na wasomi wa sheria, mtu yeyote anayekubali kufuata na kutii sheria ni mwanasheria,” amesema.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BoT YAHIMIZA UWEKEZAJI MADUKA YA KUBADILI FEDHA TANGA

    May 09, 2025
  • HISTORIA YAANDIKWA, HANDENI YAPATA CHUO CHA UUGUZI NA UKUNGA

    May 04, 2025
  • SPIKA BWZ AGAWA MITUNGI YA GESI 61 KUADHIMISHA MIAKA 61 YA MUUNGANO

    April 27, 2025
  • SPIKA BWZ ATEMBELEA MIRADI YA BILIONI 8 TANGA

    April 26, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.