TANGA YATAIFISHA, YAGAWA CHOKAA KWA TAASISI ZA UMMA
Na Zuberi Mgaya, MUM-TANGA
Serikali mkoani Tanga imekamata, kutaifisha na kugawa mifuko 1,610 ya chokaa iliyokuwa imehifadhiwa kwenye vifungashio vya kampuni ya Liemba kinyume cha sheria na taratibu.
Kampuni hiyo ni mzalishaji halali ya chokaa mkoani Tanga, iliyotoa taarifa kwenye Tume ya Ushindani kuhusu kuwepo kwa bidhaa hiyo inayohifadhiwa kwenye vifungashio vyake na watu ambao hawajajulikana.
Hivyo, baada ya Tume ya Ushindani kufanya uchunguzi, ilifanikiwa kuikamata na kuitaifisha mifuko hiyo ya chokaa, kisha kuigawa kwa taasisi 12 za umma mkoani humo.
Ugawaji huo ulifanyika kwenye bandari ya Tanga kulipohifadhiwa shehena ya chokaa hiyo iliyogawiwa na Mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Henry Sheshe.
Taasisi hizo zilizogawiwa chokaa hizo na idadi ya mifuko kwenye mabano ni Magereza mkoa wa Tanga (200), Polisi mkoa wa Tanga (100), Jeshi la Wananchi Tanzania (100),Uhamiaji (100).
Chokaa nyingine iligawiwa kwenye halmashauri za Jiji la Tanga (400), Wilaya ya Handeni (200), Mkinga (100), Pangani (100), Muheza (100), Korogwe Mjini (100), Wilaya ya Korogwe (100) na Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya ya Pangani (100).
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.