Serikali Mkoani Tanga imeridhika na ujenzi wa Kambi T15 ya Bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Chongoleani kwenye kata Mabanda Wilayani Handeni.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyakazi wa kampuni hiyo na viongozi wa Wilaya hiyo mara baada ya kukagua ujenzi huo Kambini hapo..
"Nimefurahi sana kuwa Kampuni hii ya wazawa imeanza vizuri kwa wakati na imekamilisha kazi kwa asilimia 46 hadi sasa" alisema Mgumba.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya wa Handeni Siriel Mchembe amesema kuwa mradi huo umeinua uchumi wa wananchi wa Wilaya hiyo ambapo wananchi 437 wamelipwa fidia kupisha mradi na kuajiri wananchi 170 hadi sasa.
Naye Meneja wa Mradi huo kwenye Kampuni hiyo Mhandisi Alnord Siliro amesema kazi ya ujenzi huo umegharimu Tshs. Bilioni 8.9.
" Kazi ya ujenzi ilianza Augost 12 2022 na unatarajia kukamilika Desemba 24, 2022 na kazi inaendelea vizuri" alisisitiza Meneja huyo.
Hadi sasa pamoja na kazi zake kampuni hiyo ya JV APEK tayari imeshachimba visima vikubwa viwili vya maji amabayo vinawanufaisha wananchi wa kata ya Mabanda.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.