Jamal Zuberi, Tanga.
Baraza la Wafanyakazi mkoa wa Tanga wametembelea Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi lengo likiwa ni kujionea vivutio vinavyopatikana katika hifadhi hiyo ambayo inapatikana ndani ya mkoa wa tanga sambamba na kuhamasisha wageni kuweza kutembelea vivutio hivyo.
Akizungumza Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Tanga Sebastian Masanja amesema kuwa wao kama mkoa wamemeona fahari kutembelea mbuga hiyo yenye vivutio vya pekee ambavyo ni adimu kuviona katika maeneo mengine.
“Hifadhi ya taifa ya Mkomazi ina wanyama adimu ikiwemo faru weusi ambao walikuwa hatarini kutoweka sasa leo hii tutapata bahati ya kuwaona ikiwa ni fursa ya kipekee kwetu sisi watumishi wa mkoa wa Tanga kujionea wanyama hao tena kwa ukaribu zaidi” alisema Masanja.
Aidha aliongeza kuwa huo ni mwazo ambao mkoa wameanza kutembelea hifadhi ya Mkomazi dhamira ya mkoa ni kutembelea vivutio vyote vilivyopo mkoani humo na kuvitangaza ili watu wengine waweze kuhamasika kuja kuvitembelea na kukuza utalii wetu wa ndani.
Naye Mhifadhi Mkuu kitengo cha utalii kutoka hifadhi ya taifa ya Mkomazi Happiness Kiemi ameishukuru Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga kwa kutembelea hifadhi hiyo kwa kuwa wameunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Hassan za kutangaza sekta ya utalii.
“Hifadhi ya taifa ya Mkomazi ipo katika maeneo mawili Mkoa wa Tanga na Kilimanjaro, kwa mkoa wa Tanga wageni hawa wameonyesha moja kwa moja kuunga mkono kitihada za Mhe Rais za kutangaza utalii katika nchi yetu ya Tanzania na wao wamehamasika kuja kutembelea hifadhi hii ya mkomazi” alisema Happiness.
Kwa upande wa wafanyakazi walitembelea hifadhi hiyo wamepongeza jitihada zilizofanywa na viongozi wa mkoa kuhakikisha safari hiyo inafanikiwa na kuwataka viongozi wa mikoa mingine kuja katika hifadhi hiyo na nyinginezo zinazopatikana mkoani Tanga kuweza kujifunza na kuelimika pamoja kupitia vivutio vinayvopatikana ndani ya hifadhi hizo.
Hifadhi ya Taifa Mkomazi ni moja ya kivutio cha utalii kinachopatikana ndani ya mkoa wa Tanga huku kikivutia zaidi kwa uwepo wa mandhari nzuri iliyozungukwa na milima, uwepo wa faru weusi, mbwa mwitu pamoja na wanyama wengine wengi.
Mwisho.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.