• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 171 KUTATUA CHANGAMOTO YA MAJI KOROGWE ,TANGA

Imewekwa tarehe: May 17th, 2023

Na Emma Kigombe

Serikali kupitia wizara ya Maji imeeleza mpango mkakati wa kuhakikisha unatatua changamoto ya upatikanji wa maji katika wilaya ya Korogwe, Handeni, Muheza na Pangani kupitia mradi mkubwa wa kutoa maji ya mto pangani na kuyasambaza katika maeneo hayo amboa utagharimu shilingi zaidi ya Bilioni 171.

Hayo yamebainishwa na waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso katika ziara yake ya siku moja wilayani Korogwe iliyolenga kutafuta ufumbuzi wa changamoto ya uhaba wa upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo

” Tunampango mkakati wa kutoa maji katika mto Pangani na kusambaza katika wilaya za Korogwe, Handeni, Muheza na Pangani ili  kuhakikisha wanatumia mto huo kupata maji safi na salama” alisema Aweso

Aidha Aweso ameeleza hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuhakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wakiwa wanasubiri kukamilika kwa mradi huo mkubwa ambao utaenda kuondoa changamoto ya upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo ikiwemo uchimbaji wa visima zaidi ya saba.

“Jitihada ambazo tumezifanya za muda mfupi ni uchimbaji wa visima ambavyo vitaweza kuingizwa kwenye mfumo ili wananchi wa Korogwe waweze kupata huduma ya maji safi na salama wakati wanasubiri mradi ukamilike” aliongeza Aweso

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya korogwe Joketi Mwegelo ameipongeza Serikali kwa hatua waliyochukua katika kuhakikisha wananchi wa Korogwe wanapata huduma ya maji safi na salama kwa  akihakikisha wanasimamia kwa ukaribu maagizo yote yaliyotolewa katika kutekeleza mradi huo ambao utaenda kutatua tatizo la maji wilayani humo.

“Tutaendelea kuhakikisha watumishi wa maji wanatimiza wajibu wao tunafahamu maji ni uhai na kiu kubwa ya wananchi wa Korogwe ni kuona adha ya maji inatokomea” alisema Joketi

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HISTORIA YAANDIKWA, HANDENI YAPATA CHUO CHA UUGUZI NA UKUNGA

    May 04, 2025
  • SPIKA BWZ AGAWA MITUNGI YA GESI 61 KUADHIMISHA MIAKA 61 YA MUUNGANO

    April 27, 2025
  • SPIKA BWZ ATEMBELEA MIRADI YA BILIONI 8 TANGA

    April 26, 2025
  • MILIONI 100 ZATOLEWA KUBORESHA SOKO LA NGAMIANI TANGA

    April 26, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.