Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
NI kama kusema, ‘hakuna kulala’ kwa viongozi mkoani Tanga, bali kutumia muda ipasavyo, kumsaidia Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kutekeleza majukumu na uwajibikaji kwa wananchi.
Leo Juni 30, 2025, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amewaapisha Wakuu wa Wilaya, Mhe Salum Nyamwese (Handeni) na Mhe Ayubu Sebabile (Muheza) walioteuliwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Juni 23, mwaka huu.
Akizungumza kwenye hafla ya kuwaapisha Wakuu wa Wilaya hao, Mhe Balozi Dkt Batilda, amehimiza uwajibikaji, weledi, uadilifu, uaminifu kwa viongozi hasa wa kuteuliwa na watumishi wa umma.
Akawaelekea Wakuu wa Wilaya kushiriki ipasavyo katika utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais Dkt Samia, ikiwemo kutatua kero za wananchi, watumishi, matumizi ya mifumo katika ukusanyaji mapato na udhibiti wa matumizi yasiyofaa ya fedha za umma.
Mhe Balozi Dkt Batilda, amesisitiza umuhimu wa kuwafikia wananchi, kwa kuwataka Wakuu wa Wilaya mkoani humo, kuendeleza ziara mahususi za utatuzi wa kero kesho Julai Mosi, 2025 na kutenga siku maalumu za kazi hiyo kwenye ofisi zao.
Pia, Mhe Balozi Batilda amesema Wakuu wa Wilaya hao wanapaswa kusimamia kwa nguvu masuala ya ulinzi na usalama wa watu na mali zao, na kudhibiti viashiria vya uvunjifu wa amani kwa jamii.
Amevitaja baadhi ya viashiria hivyo ni migogoro ya ardhi ikiwemo ya wakulima na wafugaji na wanaodai fidia mbalimbali.
Piam Mhe Balozi Dkt Batilda amesema Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wanapaswa kutambua uzito na heshima walizopewa kupitia uteuzi, hivyo kuzitendea haki kwa uadilifu na utendaji kazi wenye tija.
AAGIZA KILA KAYA KUPANDA MIGOMBA 10 MUHEZA
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, mipango ya kuifanya Tanga kurejea kuwa ya viwanda, kadri ya nia ya Mhe Rais Dkt Samia aliyoitangaza katika ziara yake mkoani humo Februari 28, 2025.
Amemuelekeza Mhe Sebalile, kusimamia suala la viwanda vikiwemo vya kusindika viungo, juisi, jam na upandaji migombona utaowezesha kila kaya kupata na kupanda mbegu za mikakao 10.
UMAKINI KATIKA KUTUNGA SHERIA NDOGO ZA HALMASHAURI
Mhe Balozi Dkt Batilda, amewaelekewa Wakuu wa Wilaya kuhamikisha mchakato wa utungaji sheria ndogo za halmashauri, unafuata kanuni na taratibu ikiwemo kuwashirikisha wadau, kabla ya kuzipeleka kwenye mamlaka za utiaji saini ili kuidhinishwa kwa matumizi.
Amesema, hali hiyo itaziepusha halmashauri za mkoani humo dhidi ya sheria ndogo zinazokinzana na mahitaji ya wananchi, wakiwemo wadau katika sekta mbalimbali na hivyo kuibua migogoro isiyokuwa na tija.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.