Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
UTEUZI na mabadiliko ya viongozi mbalimbali yaliyofanywa Juni 23, 2025 na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ’yamemgusa’ aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa (RAS) wa Tanga, Pili MnyemaN(pic, anayehamia mkoa wa Pwani.
Mnyema anachukua nafasi ya Rashid Kassim Mchata, aliyekuwa Katibu Tawala Mkoa wa Pwani ambaye anahamia Tanga. Ni sawa na kusema, mabadiliko hayo yamewafanya wawili hao ’kubadilishana’ vituo vya kazi.
Mnyema aliteuliwa kuwa RAS wa Tanga Mei 29, 2021 na kuapishwa Juni 2, 2021 saa 4:00 asubuhi, Ikulu Chamwino jijini Dodoma, pamoja naye, wakiwemo wateuliwa kadhaa wa nafasi hiyo, miongoni mwao ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, aliyeteuliwa kuwa RAS wa Shinyanga.
Baadaye yaani Julai 28, 2022, Balozi Dkt Batilda aliteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Machi 9, 2024 akahamishiwa mkoa wa tanga anapoendelea na wadhifa huo hadi sasa.
Mbali na Mnyema, viongozi wengine mkoani Tanga walioguswa na mabadiliko hayo ni aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe Japhari Kubecha aliyehamishiwa wilaya ya Gairo, Katibu Tawala Wilaya (DAS) ya Tanga, Mikaya Dalmia anayekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni.
Mwingine ni aliyekuwa Afisa Elimu Mkoa (REO) wa Tanga, Newaho Mkisi, aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.