• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

BALOZI BATILDA ASEMA TANGA INA HIFADHI YA LITA ZA UJAZO MILIONI 210 ZA MAFUTA

Imewekwa tarehe: July 17th, 2025

Na Mashaka Mgeta, DODOMA

UWEKEZAJI mkubwa uliofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye sekta ya nishati, umeuwezesha Mkoa wa Tanga kuwa na hifadhi ya lita za ujazo milioni 210 za mafuta ya petroli na dizeli.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amesema hayo juzi Julai 15, 2025, alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Kikao hicho ni sehemu ya utaratibu wa Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, kuwaalika Wakuu wa Mikoa kuelezea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia.

Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, kiasi hicho cha mafuta kinachohifadhiwa kwenye tenki za mafuta za kampuni ya GBP, kinakidhi matakwa ya kanuni za nishati hiyo na maagizo ya Mhe Rais Dkt Samia, kusambazwa kwenye mikoa ya Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.

Amesema usambazi wa mafuta kutokea mkoani Tanga, kunachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za usafirishaji kwa wafanyabiashara, hivyo bei kuwa rafiki kwa watumiaji.

Mhe Balozi Dkt Batilda amesema hifadhi hiyo ya mafuta, ni sehemu ya fursa nyingi za kiuchumi zilizopo na zinazoendelea kukua mkoani Tanga, tangu Mhe Rais Dkt Samia kuingia madarakani 2021.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, Tanga inaendelea kutoa elimu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi, taasisi za Serikali na zisizo za kiserikali. 

Kwa mujibu wa Mhe Balozi Dkt Batilda, hadi sasa taasisi 1,493 za Serikali zenye watumiaji 735,372 wa nishati safi ya kupikia zimetambuliwa.

BOMBA LA MAFUTA GHAFI 

Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, Mradi wa Bomba na Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP) wenye urefu wa kilomita 205.91 unaohusisha ujenzi wa kituo cha kupokelea, kuhifadhi na kusafirisha mafuta, usimamizi na uendeshaji wa mradi na matenki manne, umekamilika kwa asilimia 53.

Amesema, fidia kwa wakazi waliopisha mkuza wa EACOP mkoani Tanga umefikia asilimia 98.7 ambapo kati ya wananchi 1560 kati ya wanufaika1580 wameshapokea malipo ya fidia inayofikia Shilingi billion 9.38. 

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • WAANDISHI DODOMA WAVUTIWA NA MAENDELEO YA TANGA, WAALIKWA KUFANYA ZIARA

    July 17, 2025
  • RC BATILDA:ONGEZEKO LA WATU TANGA ISHARA YA UBORA WA HUDUMA ZA FYA, USTAWI WA JAMII

    July 17, 2025
  • TANGA TUNA UTOSHELEZI WA CHAKULA - BALOZI BATILDA

    July 17, 2025
  • BALOZI BATILDA ASEMA TANGA INA HIFADHI YA LITA ZA UJAZO MILIONI 210 ZA MAFUTA

    July 17, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.