Na Mashaka Mgeta, DODOMA
HISIA zilizohifadhiwa kwenye mtima wao ziliwazidi, wakafunguka, wakacheka, wakafurahi baada ya kusikia taarifa ya maendeleo ya Mkoa wa Tanga katika kipindi cha utawala wa Awamu ya Sita wa Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Hao ni Waandishi wa Habari waliohudhuria mkutano ulioitishwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, kuzungumza nao jijini Dodoma jana Julai 15, 2025.
Baada ya uwasilishaji wa taarifa ya Mhe Balozi Dkt Batilda kisha kupokea maswali na kuyajibu kwa kina, Waandiishi wa Habari walionesha nyuso za bashasha, wakifurahia na wengine wakisikika kusema, “Tanga mnatisha.”
Hali hiyo inamuibua Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Jonas Kamaleki aliyeongoza mjadala huo, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, Kamaleki akasema, furaha iliyooneshwa na Waandishi wa Habari baada ya hotuba ya Mhe Balozi Dkt Batilda, ni ishara ya kukubalika na kada hiyo umuhimu katika sekta ya habari mawasiliano.
Kwa maelezo hayo, Mhe Balozi Dkt Batilda akawashukuru Waandishi wa Habari na kuwapa mwaliko wa kufanya ziara ya kikazi mkoani Tanga, ili kujionea hatua kubwa za maendeleo zilizopigwa katika utawala wa Mhe Rais Dkt Samia.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.