Na Mashaka Mgeta, DODOMA
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amethibitisha kuwepo utoshelezi wa chakula mkoani humo, unaotokana na maboresho ya sekta ya kilimo yaliyofikiwa katika Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Mhe Balozi Dkt Batilda ameyasema hayo juzi Julai 15, 2025, alipokuwa akizungumza kwenye Mkutano wa Waandishi wa Habari ulioandaliwa na Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali jijini Dodoma.
Amesema, katika kipindi cha takribani miaka minne ya uongozi wa Mhe Rais Dkt Samia, Tanga imepokea Shilingi bilioni 33.3 kwa shughuli za kilimo.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, miongoni mwa mafanikio yaliyotokana na uwekezaji huo ni kutolewa kwa pembejeo za ruzuku kama vile mbegu bora na mbolea kwa wakulima 134,527 waliosajiliwa kidigitali.
Wakulima 11,198 walinufaika na tani 4,235.35 za pembejeo kwa gharama ya Shilingi bilioni 8.1 huku ruzuku ya Serikali ikiwa ni Shilingi bilioni 2.5.
Pia, amesema pikipiki 380 zenye thamani ya Shilingi milioni 950, vishikwambi 371 vya ukusanyaji takwimu (Shilingi milioni 296.8) na vipima odongo saba (Shilingi milioni 153) kwa upimaji na ushauri wa kitaalamu kwa wakulima vimetolewa mkoani humo hivyo kuongeza ubora na wingi wa uzalishaji mazao.
“Hali ya chakula mkoani Tanga na nzuri na toshelezi,” amesema na kutoa mfano kuwa, msimu wa 2023/24, kilimo kilifanyika kwenye jumla ya hekta 909,076 za mazao ya chakula, na kuzalisha tani 2,659,802 (ghafi), sawa na tani 1,314,292.4 za chakula kikavu. “Uzalishaji huu umetosheleza mahitaji ya wakazi wapatao 2,615,597 wa mkoa huu, na kuwa na ziada ya chakula kwa ajili ya biashara na hifadhi,” amesema.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.