Na Mashaka Mgeta, DODOMA
UHAKIKA wa huduma bora za afya na ustawi wa jamii hasa kwa masuala ya uzazi salama, ni miongoni mwa maeneo muhimu yanayochangia ongezeko la watu mkoani Tanga.
Waandishi wa Habari mkoani Dodoma wanaguswa na hali hiyo, hivyo kutaka kujua kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian aliyezungumza nao jana Julai 15, 2025 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali.
Bilson Vedastus wa Nyemo FM Radio, ni sehemu ya waandishi waliouliza maswali kwenye mkutano huo, akirejea tukio la baadhi ya wanawake wa kijiji cha Mwembeni, kata ya Madanga wilayani Pangani, kudai hawatabeba mimba kutokana na kutokuwepo zahanati.
Madai hayo waliyatoa Julai 4, 2024 walipokutana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Tanga, Rajab Abdulrahman aliyekuwa katika ziara ya kukagua miundombinu ya afya wilayani Pangani.
Vedastus alitaka kujua kama hitaji la wanawake hao kuhusu ujenzi wa zahanati limefikiwa, na ikiwa wana msimamo huo ama wameridhia kuendeleza mgomo wa kutobemba mimba.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, Serikali na wakazi wa Mwembeni, walishaanza ujenzi wa zahanati.Jengo hilo ambalo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga, Abdulrahman alichangia Shilingi milioni 12 lipo katika hatua ya umaliziaji, kama linavyoonekana kwa picha zilizoambatanishwa kwenye habari hii.
Pia, Mhe Balozi Dkt Batilda akasema, mpango wa M-Mama wa Mhe Rais Dkt Samia, unaoruhusu kufanikisha usafiri rafiki usiokuwa wa magari ya wagonjwa, kumfikisha mjamzito kituo cha huduma, unatekelezwa kwa ufanisi na kuwa kishawishi kwa wanawake kupata ujauzito pasipo hofu.
Amesema, zipo ishara nyingi zinazohusu nafasi ya huduma bora za afya na ustawi wa jamii, kuchangia ongezeko la asilimia 2.5 kwa mwaka la wakazi Tanga, ambao kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya 2022, walikuwa 2, 615,597.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.