Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amewaasa viongozi wa dini kudhibiti na kukemea matendo maovu yanayochangia upotevu wa amani, umoja na mshikamano nchini.
Mhe Balozi Dkt Burian, ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye Iftar aliyowaandalia viongozi wa dini jijini Tanga, Machi 29, 2025.
Amesema, pamoja na jukumu msingi ya viongozi hao kuombea amani ya nchi, wanapaswa, kila wanapobaini ukiukwaji wa misingi ya haki na umoja, wakemee kwa nguvu zote ili amani na mshikamano vidumu nchini.
"Niwaombe viongozi wa dini kuendelea kuombea amani ya nchi, lakini mtakapowabaini watu wenye nia ovu ya kuanzisha chokochoko, ni vema mkawaonya na kuishirikisha Serikali ili tuweze kuwadhibiti,"amesema Mhe Balozi Dkt Batilda.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Tanga, Sheikh Juma Luuchu amewataka waumini wa dini zote kuendeleza matendo mema waliyoyashiriki kipindi cha mfungo wa Ramadhani na Kwaresma.
Alisema waumini hao wanapaswa daima, kudumisha amani hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge, Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani utakaofanyika baadaye mwaka huu.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.