• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

RC TANGA ATAJA MAENEO YA USHIRIKIANO NA MAHAKAMA

Imewekwa tarehe: February 2nd, 2026

 

Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, ameahidi kuratibu mpango wa kupata rasilimali zitakazoboresha huduma kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Tanga, ikiwemo usikilizaji mashauri kwa njia ya mtandao.

Mhe Balozi Dkt Batilda ameyataja maeneo mengine ya uratibu ni upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa mahakama na ofisi zake, ili kuwafikishia wananchi huduma za kimahakama kwa karibu zaidi.

Ameyasema hayo leo Februari 2, 2026 kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria, yenye kauli mbiu inayosema, “Mchango wa mahakama katika ustawi na maendeleo ya Taifa”, na kuongeza kuwa, uratibu huo ni mwendelezo wa ushirikiano usioathiri uhuru wa mihimili ya Bunge, Mahakama na Serikali.

Mhe Balozi Dkt Batilda amasema, kufanyika kwa maadhimisho hayo ni ishara ya wazi kwamba Tanzania inatambua na kuheshimu utawala wa sheria, kadri ulivyoakisiwa kwenye Katiba ya nchi.

Kwa upande mwingine, Mhe Balozi Dkt Batilda, amesema mahakama inachangia kustawisha maendeleo ya nchi kwa njia tofauti kama vile utatuzi wa migogoro ikiwemo ya ardhi.

Amesema, hali hiyo inawafanya wadaawa kupata haki kwa wakati, hivyo kutekeleza majukumu yao ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na nchi kuendelea kunawiri katika nyanja zote.

Kwa mujibu wa Mhe Balozi Dkt Batilda, ongezeko la thamani ya ardhi na kukua kwa uelewa wa thamani ya rasilimali hiyo, ni miongoni mwa vichocheo vya migogoro ya ardhi mkoani humo.

Naye Mwanasheria Mkuu wa Mkuu wa Serikali, Hamza Saidi Johari amepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025.

Kupitia hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Mwanasheria wa Serikali Mkoa wa Tanga, Wakili Rebecca Msalangi, Johari amesema hatua hizo hususani kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi, kutaweka msingi wa maridhiano ya kitaifa, kujenga na kudumisha umoja na mshikamano nchini.

Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amesema TLS iko tayari kushirikiana na Serikali na wadau wote kutafuta suluhu endelevu ya changamoto zinazohitaji nguvu ya pamoja kuleta ustawi wa maendeleo kitaifa.

 

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • JAJI MFAWIDHI TANGA ANENA: MIFUMO IMEDHIBITI RUSHWA, UKIRITIMBA MAHAKAMANI

    February 02, 2026
  • RC TANGA ATAJA MAENEO YA USHIRIKIANO NA MAHAKAMA

    February 02, 2026
  • COPRA YAGAWA TANI 1.35 YA MBEGU ZA UFUTA TANGA

    January 30, 2026
  • BAADA YA RS TANGA: SAADANI YAZIITA TAASISI KUFANYA VIKAO KWENYE HIFADHI

    January 30, 2026
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.