Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
UNAPOTAJA hatua za maendeleo katika sekta tofauti nchini, kwa wasioukubali ukweli, wanaweza kudhani ni hadithi za kufikirika.
Mkoani Tanga, yapo mambo mengi yanayodhihirisha kipimo kikubwa cha maendeleo yanayotokana na ubora wa miundombinu na huduma kwa jamii, yaliyofikiwa kupitia Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Wakati wakazi wakiyapokea na kuyaishi mafanikio hayo, Mwenge wa Uhuru 2025 unafika mkoani humo, na ukiwa katika Halmashauri ya Jiji la Tanga, unatembelea, kukagua na kuzindua awamu ya kwanza ya mradi wa ufungaji wa dira za maji za malipo ya kabla ya matumizi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ali Ussi, anashiriki shughuli hizo kwa mradi huo unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) kwa gharama ya Shilingi bilioni 1.9.
Kwa mujibu wa taarifa ya Tanga UWASA kwa Mwenge wa Uhuru, mradi hu oni utekelezaji wa maagizo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kuhusu ufungaji wa dira za maji za malipo ya kabla kwa wananchi, ili kuboresha upatikanaji wa huduma husika kwa wakazi wa jijini na maeneo ya Muheza na Pangani.
Mradi huo ulianza kutekelezwa Julai mwaka jana, kwa fedha za Serikali Kuu kupitia Wizara ya Maji, chini ya Programu ya IFF-OBA (Investment Financing Facility – Output Based Aid) na Mfuko wa Maji wa Taifa (NWF).
Taarifa ya Tanga UWASA inaeleza kuwa mradi hadi umefikia asilimia 55.05 kwa kufunga dira 2,202 kati ya 4,000 zinazostahili.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.