• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MWENGE WAONYA: MSIHARIBU MIUNDOMBINU, SERIKALI HAIJALALA

Imewekwa tarehe: June 17th, 2025

Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ali Ussi, amewatahadharisha watu wenye nia ovu, wanaopanga ama kutekeleza vitendo vya uharibifu wa miundombinu ya sekta mbalimbali za maendeleo na huduma nchini.


Ussi ametumia fursa ya kutembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi ama kuzindua miradi iliyofikiwa na Mwenge wa Uhuru 2025 mkoani Tanga, kutahadharisha, kutokana na ubora, ukubwa wa thamani na umuhimu wake kwa jamii pana.Amesema Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha takribani miaka mitano, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutekeleza ujenzi wa miundombinu kama barabara, makalavati, madarasa, vyumba vya mionzo, zahanati, nyumba na ofisi za watumishi wa umma, miongoni mwa mingine mingi.


Akizungumza baada ya kukagua mradi wa ofisi ya Kata ya Tongoni katika Halmashauri ya Jiji la Tanga jana Juni 16, 2025, Ussi, amesema watu wenye nia za kupanga ama kushiriki vitendo hivyo hawana budi kujitafakari na kuondokana na azma hizo, kwani Serikali iliyopewa dhamana na umma kusimamia rasilimali zote, haijalala. 


Taarifa ya Halmashauri ya Jiji la Tanga ilieleza kuwa, Shilingi milioni 85 zimetolewa kupitia mapato ya ndani kwa ujenzi wa ofisi hiyo ulioanza Oktoba 1, 2023 na kutakiwa kukamilika Disemba 29, 2023.


Hata hivyo, mradi huo haukukamilika kutokana na changaoto mbalimbali ikiwemo uwepo wa jengo la zahanati ya zamani eneo la mradi, fedha za mradi awamu ya kwanza kuisha na fundi wa mradi kuugua. Mradi huo umetekelezwa kwa kutumia njia ya "Force account" na manunuzi kupitia mfumo wa NeST, ulitumika kwenye manunuzi ya baadhi ya vifaa na baadhi ya vifaa vilinunuliwa kabla ya mfumo wa NeST haujaanza.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BALOZI BATILDA AHIMIZA UMOJA, MSHIKAMANO TANGA

    June 18, 2025
  • RAS TANGA 'AWASHUKIA' WATUMISHI WANAOISHI NJE YA VITUO VYA KAZI

    June 18, 2025
  • BILIONI 1.9 ZINAVYOIINGIZA TANGA KWENYE MALIPO YA KABLA YA MATUMIZI YA MAJI

    June 17, 2025
  • MWENGE WAONYA: MSIHARIBU MIUNDOMBINU, SERIKALI HAIJALALA

    June 17, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.