• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

BOMBA LA MAFUTA

Imewekwa tarehe: October 25th, 2022

SERIKALI Mkoani Tanga imesema maandalizi ya awali ikiwemo utafiti wa udongo katika maeneo yatakayowekwa miundombinu ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki kutoka Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga, yanaendelea vizuri.

Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, waliomtembelea ofisini kwake Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba amesema tayari maeneo kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya kambi mkoani hapa inaendelea vizuri ikiwemo fidia kwa wananchi kupisha ujenzi wa bomba imeshatolewa.

“Mradi unaendelea kwa kasi naamini utakamilika kwa wakati kama yalivyo matarajio ya serikali na wananchi,” amesema Mgumba.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Daniel Sillo ameishauri serikali kuhakikisha inasimamia kwa ukaribu utekelezaji wa mradi  ili ukamilike kwa wakati na kuleta tija ya kiuchumi kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

“Kamati tumeridhishwa na jitihada kubwa ambazo serikali imechukua ikiwemo maandalizi mbalimbali ya ujenzi wa mradi huo ambao ukikamilika utafungua fursa za kiuchumi za nchi yetu,” amesema Sillo.

Naye Msimamizi wa mradi huo Safiel Msofe, amesema mradi huo umezingatia taratibu za kimataifa za fidia hivyo watahakikisha wananchi wanapata stahiki zao za fidia kwa mujibu wa taratibu zilizopo.

“Wananchi 388 tayari hadi sasa wameshalipwa fidia ya TShs Bilioni 2.4, kupisha maeneo yao yatayopitiwa na miundombinu ya ujenzi huo.

“Kwa sasa wananchi 6,134 ambao wapo kwenye eneo la mkuzi taratibu zinaendelea za kuhakikisha nao wanalipwa fidia zao kupisha maeneo yao tayari kwa utekelezaji wa mradi huo,” alisisitza zaidi.

Mwisho.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SARUJI TANGA YAKABIDHI BAJAJI ZA UMEME 10 KWA BALOZI BATILDA

    July 03, 2025
  • RC TANGA ASULUHISHA MGOGORO WA ARDHI TAFSIRI HASI YA RAMANI IKITAJWA CHANZO

    July 03, 2025
  • RAS MCHATTA: SINA MANENO MENGI, NIPIMENI KWA KAZI, UWAJIBIKAJI

    June 30, 2025
  • BALOZI BATILDA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIKILIZA KERO, AWAAPISHI WAWILI TANGA

    June 30, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.