• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

CCM TANGA YATETA SAFARI ZA RAIS SAMIA NJE YA NCHI

Imewekwa tarehe: May 16th, 2025


Na Mashaka Mgeta, LUSHOTO

MZAZI mwenye familia yenye mahitaji ya msingi ili ‘maisha yaendelee’, hawezi kuketi ndani akilala na kulalama, bali anatoka nje kwenda kutafuta, ili riziki ipatikane kwa njia halali.

Huo ni mfano unaotolewa na Katibu wa Mkoa wa Tanga wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mfaume Kizigo, akielezea maana na umuhimu wa safari za nje anazokwenda Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, kwa maslahi mapana ya nchi na watu wake.

Kizigo ameyasema hayo wakati Kamati ya Siasa ya Mkoa huo, ilipokagua miradi ya maendeleo wilayani Lushoto Mei 15, 2025, na kufika kwenye Shule ya Amali Shita, iliyopo kata ya Mwangoi, inayojengwa kwa gharama ya Shilingi milioni 584.3 zilizotolewa na Benki ya Dunia (WB).

Amesema, mradi huo ni miongoni kwa ushahidi kuwa kama Mhe Rais Dkt Samia ‘angejifungia ndani’ pasipo kwenda kuzungumza na WB, ingekuwa vigumu kukamilisha shule hiyo kwa wakati, hivyo kuendeleza kadhia ya watoto wa familia nufaika, kutembea umbali mrefu.

“Katika uhalisia uliopo, mahitaji yetu ndio yanayomfanya Mama (Mhe Rais Dkt Samia) asafiri nje ya nchi, na matunda yake ni kama ujenzi wa shule hii,” amesema na kushangiliwa na wakazi wa kata hiyo waliomlaki.

Kizigo amesema ni wajibu msingi wa Watanzania kuendelea kumuunga mkono, kumtia shime, kumpenda na kumuombea mema Mhe Rais Dkt Samia.

Wakazi wa Mwangoi, wamemshukuru Mhe Rais Dkt Samia, miongoni mwao ni Zubeda Juma, anayesema uwepo wa shule hiyo utaongeza ari ya kusoma na kupunguza mwendo mrefu kwa watoto wao kutembea.

Naye Bakari Twaha amesema, pamoja na manufaa hayo katika ustawi wa watu, mradi wa shule hiyo umewawezesha kupata ajira zilizowapata kipato cha kumudu kuzitunza familia zao.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • BALOZI BATILDA AHIMIZA UMOJA, MSHIKAMANO TANGA

    June 18, 2025
  • RAS TANGA 'AWASHUKIA' WATUMISHI WANAOISHI NJE YA VITUO VYA KAZI

    June 18, 2025
  • BILIONI 1.9 ZINAVYOIINGIZA TANGA KWENYE MALIPO YA KABLA YA MATUMIZI YA MAJI

    June 17, 2025
  • MWENGE WAONYA: MSIHARIBU MIUNDOMBINU, SERIKALI HAIJALALA

    June 17, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.