• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

TAHADHALI: ASILIMIA 60 YA UBORA WA NGOZI INAPOTEA KWENYE KUCHUNA

Imewekwa tarehe: May 29th, 2025

Na Emma Kigombe, OMM TANGA

TAFITI zinaonesha kuwa kati ya asilimia 45 hadi 60 ya uharibifu wa ngozi inatokea wakati wa uchunaji ngozi kwenye machinjio, jambo linalochangia kwa kiasi kikubwa kushuka kwa ubora na thamani ya zao hilo muhimu kwa uchumi wa taifa.

Hayo yamebainishwa wakati wa ufunguzi wa mafunzo maalum kwa wakaguzi wa ngozi kutoka mikoa ya Tanga na Kilimanjaro, yaliyofanyika leo jijini Tanga kwa lengo la kuboresha mnyororo wa thamani wa zao hilo, kupitia usimamizi bora wa hatua zote za uzalishaji.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkuu wa Idara ya Uchumi na Uzalishaji katika Sekretarieti ya Mkoa wa Tanga, George Mmbaga, amesema wachunaji ngozi ya wanyama wana mchango mkubwa katika kudhibiti ubora wa ngozi, hivyo ni muhimu kuwajengea uwezo kupitia mafunzo ya kitaalamu ya uchunaji bora.

Pamoja na mafunzo hayo, washiriki wamepewa vitendea kazi kama vile vitambulisho na nakala za sheria na kanuni za ngozi, ili kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa.

Katika juhudi za kuinua tasnia ya ngozi nchini, Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa koo za mifugo kupitia uhimilishaji na usambazaji wa madume bora, ukarabati wa majosho 762 na utoaji wa ruzuku ya dawa za kuogeshea mifugo.

Mikakati mingine ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wachunaji 2,263, wapanga madaraja wa ngozi 75 na wakaguzi wa ngozi 113 na kugawa visu vya kisasa kwa ajili ya uchunaji bora.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • UTENZI: KARIBU MWENGE WA UHURU MKOANI TANGA - JULAI 6, 2025

    May 31, 2025
  • TAHADHALI: ASILIMIA 60 YA UBORA WA NGOZI INAPOTEA KWENYE KUCHUNA

    May 29, 2025
  • TANGA WAASWA KUENDELEZA UKAGUZI, UTUNZAJI MIRADI BAADA YA MWENGE WA UHURU

    May 29, 2025
  • WATOKA NYUMBANI 'PATUPU', WAREJEA NA MILIONI 3, MAJIKO YA GESI YA RC TANGA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.